Kituo cha uratibu wa pamoja wa usafirishaji wa chakula cha Ukraine chaanzishwa katika Uturuki

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2022
Kituo cha uratibu wa pamoja wa usafirishaji wa chakula cha Ukraine chaanzishwa katika Uturuki
Picha iliyopigwa Tarehe 27, Julai, 2022 ikionesha Kituo cha Uratibu wa Pamoja kilichoko Istanbul, Uturuki. (Picha/Xinhua)

Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar aliwaambia waandishi wa habari kuwa, Jumatano wiki hii Waturuki walianzisha kituo cha uratibu wa pamoja huko Istanbul, ili kufuatilia na kusimamia hali ya usafirishaji wa chakula cha Ukraine.

Akar alisema, kituo hicho kiko ndani ya ua wa chuo kikuu cha kijeshi cha eneo la Besiktas lililoko upande mmoja wa Ulaya wa mji huo, na kimeundwa na wajumbe 20 kutoka Russia, Ukraine, Uturuki na Umoja wa Mataifa, na kila upande una wajumbe watano.

Waziri huyo alisema, kituo hicho kitahakikisha njia salama kwa meli kutoka bandari ya Ukraine kupita Bahari Nyeusi na mlango bahari wa Bosphorus wa Istanbul kuingia soko la dunia nzima.

Alisema, meli ya kwanza inayobeba nafaka inafanya maandalizi ya kuondoka Bandari ya Ukraine.

“Tunaamini kazi ya kituo cha uratibu wa pamoja itatoa mchango mkubwa kwa ajili ya kushinda msukosuko wa chakula unaoathiri dunia nzima na kupunguza bei za chakula,” alisema Akar.

Ijumaa ya wiki iliyopita Russia na Ukraine zilisaini “ Makubaliano ya kusafirisha mazao ya kiliomo ya Bahari Nyeusi”, makubaliano hayo yanaruhusu Ukraine kusafirisha kiasi kikubwa cha chakula na mbolea kutoka bandari tatu kuu za Bahari Nyeusi, yaani Bandari ya Odessa, Chernomorsk na Yuzhny.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha