Uchoraji wa Picha za wanyama za 3D umekuwa hatua mpya ya kuhifadhi miti (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 29, 2022
Uchoraji wa Picha za wanyama za 3D umekuwa hatua mpya ya kuhifadhi miti

Tarehe 26, Julai, 2022, wasanii walichora picha za wanyama za 3D kwenye matundu na majeraha ya miti kwenye mtaa wa Guling wa Lushan mjini Jiujiang, Mkoa wa Jiangxi. Picha hizi za wanyama mbalimbali zimevutia watalii wengi kuangalia.

Wahuduma wa ofisi ya eneo la vivutio la Mlima Lu walijulisha kuwa, baadhi ya miti kwenye kando mbili za barabara imeliwa na wadudu au imekuwa na dalili ya kuoza. Ili kutatua matatizo hayo, wafanyakazi wameshughulikia kwa makini na kupaka dawa kwenye matundu ya miti, na kuwaalika wasanii kuchora picha kwenye sehemu za matundu na majeraha hayo ya miti kwa kutumia rangi zinazoweza kuzuia maji na hali joto ya hewa. Hatua hizi siyo tu zimehifadhi miti, bali pia zimelifanya eneo la vivutio kuwavutia sana watalii kutokana na sanaa za picha za wanyama za 3D zilizochorwa na wasanii.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha