Rekodi mpya! Uundaji wa Meli kubwa zaidi ya kontena duniani wakamilika Shanghai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 02, 2022
Rekodi mpya! Uundaji wa Meli kubwa zaidi ya kontena duniani  wakamilika Shanghai
Rekodi mpya! Uundaji wa Meli kubwa zaidi ya kontena duniani ukikamilika Shanghai. (Mpiga picha:Zhang Liang)

Agosti Mosi , uundaji wa meli ya kontena inayoweza kubeba makontena 24116 iliyoundwa kwenye Kituo cha uundaji wa meli cha Hudong Zhonghua cha Kundi la Meli la China umekamilika katika kituo chake cha Changxing. Meli hiyo ya kontena ni meli ya kwanza inayoweza kubeba makontena mengi zaidi duniani ambayo inaashiria kuwa uundaji wa meli kubwa ya kontena umeingia katika zama mpya zinazoongozwa na uundaji wa meli za China.

Urefu wa jumla wa meli ya aina hii ni mita 399.99, upana wake ni mita 61.5 na kimo chake ni mita 33.2, ambayo inaweza kubeba makontena 24116 kwa usafirishaji mmoja, hii ni rikodi mpya zaidi, ambayo imeonesha kuwa meli hii kweli ni kubwa zaidi na inayobeba makontena mengi zaidi kwenye bahari kuliko meli nyingine zote kwa hivi sasa.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha