Mikakati ya Mkoa wa Shaanxi wa China wa kustawisha vijiji yatoa somo la kutokomeza umaskini (5)

By Aris (Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 03, 2022
Mikakati ya Mkoa wa Shaanxi wa China wa kustawisha vijiji yatoa somo la kutokomeza umaskini
Mwonekano wa ndani wa sehemu ya watoto ya maktaba ya Kijiji cha Zhongxigou, kilichoko eneo la Liuba, katika Mji mdogo wa Huoshaodian, Mkoa wa Shaanxi wa China (Picha na People’s Daily Online)

Kwa kipindi cha muda mrefu huko nyuma, maendeleo ya China yalikuwa yamejikita katika maeneo ya mijini hususani miji mikubwa na kuviacha vijiji nyuma. Hata hivyo, Serikali ya China haikuwa imetupa macho yake nyuma, miaka michache baadaye, Rais Xi Jinping wa China alitangaza mikakati ya kuwasaidia watu wa vijijini kuondokana na umaskini, na kutangaza kampeni kubwa ya ustawishaji na upendezeshaji wa vijiji.

Mkoa wa Shaanxi nchini China ni miongoni mwa mikoa kote nchini China ambayo imepokea na kutekeleza agizo hilo la Serikali Kuu ya China na hakika namna mipango yake mbalimbali ilivyotekelezwa katika kustawisha vijiji, kuongeza mapato ya wanavijiji na kuondoa umaskini, inatoa somo muhimu katika kuondoa umaskini duniani.

Ukiwa ni Mkoa ambao ni chimbuko la Njia ya Hariri na sasa umepokea Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Mkoa Shaanxi umetekeleza mikakati mbalimbali ya kustawisha vijiji na kuondoa umaskini.

Miradi mbalimbali vijijini

Mkoa wa Shaanxi ulioko kwenye maeneo ya milima umeanzisha miradi mbalimbali vijijini na katika miji midogo. Miradi hiyo ni pamoja na ufugaji wa samaki na mazao ya majini , kilimo, utengenezaji wa sanaa za ufundi, utalii wa vijijini hususani wa kilimo, mbuga za kuhifadhi wanyama, michezo na kadhalika.

Mathalani katika Kijiji cha Zhongxigou, kilichoko eneo la Liuba, katika Mji mdogo wa Huoshaodian, kuna miradi ya shamba la kufuga nyuki wa kuzalisha asali, shamba la kuku, mashamba ya kiikokolojia hususani uoto wa maua, uunganishaji wa shughuli za utalii na kilimo, kujenga miradi ya mfano ya utalii na jumba la ufundi lenye miradi kama vile ya utengenezaji samani na maktaba kubwa iliyosanifiwa kijadi. Habari kutoka katika kijiji hicho zinaeleza, Mkoa wa Shaanxi umetoa kibali cha kuanzisha miradi ya ustawishaji kijiji ambayo inachanganya uhalisia wake ili kuunda muundo wa ukuzaji wa shughuli za utalii kwa "msingi mmoja, pete moja, ukanda mmoja" ikilenga kuimarisha aina za bidhaa, kuboresha mazingira kwa ajili ya watu kuja kufanya mapumziko ya likizo, na kuboresha huduma za utendaji na kujitahidi kujenga hoteli za watalii na maeneo ya mandhari yenye "mazingira mazuri, usafi, vifaa kamili, usimamizi sanifu, huduma ya daraja la kwanza, usalama na ustaarabu".

Kwa mujibu wa Liang Weiqi, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni na Utalii wa eneo la Liuba, miradi hiyo kwa sasa imeajiri karibu watu 4000. Anasema, huko nyuma miaka ya 2000, ni watu 1000 tu walikuwa wamejiajiri kwenye sekta hizo za vijijini. Hata, wanakijiji waliokuwa wameondoka eneo hilo kwenda mijini kutafuta vibarua na kazi nyingine sasa wameanza kurejea.

“Miaka ya hivi karibuni maendeleo yamekuwa makubwa sana, sasa kuna wafanyakazi wahamiaji wameamua kurudi nyumbani” anasema Liang.

Aidha, maeneo kama ya Changgan, Yangxian na Qinling yameanzisha shughuli za kazi za mikono kwa wakaazi na uanzishwaji wa bustani za wanyama na ndege.

Miradi yote hiyo inatajwa kuwa na manufaa makubwa kwa wakazi kupitia kutoa nafasi za ajira, kuwaongezea kipato na kukidhi mahitaji yao muhimu ya kila siku. Aidha, kutokana na kuanzishwa kwa miradi hiyo, kumekuwa na ongezeko la shughuli za kibiashara za pembezoni zinazolenga kuhudumia watalii.

Mradi wa kukuza vipaji vya mpira wa miguu

Katika mji mdogo wa Liuhou, ulioko eneo la Liuba katika Mkoa wa Shaanxi kuna mradi mkubwa wa kukuza vipaji vya mpira wa mguu wa Yingpan. Mradi huo ambao pia ni Shule ya Liuba ni mkubwa na wa aina yake umevutia mamia ya watoto na vijana kutoka maeneo mbalimbali ya China na unaelezwa kuanza kuzaa matunda katika kuwaandaa wachezaji wa Timu ya Taifa ya China.

Wasimamizi wa mradi huo wamesema kuwa, tayari umeshatoa majina ya wachezaji wa kike kushiriki kwenye kambi ya mazoezi ya Timu ya Taifa ya China ya Wanawake kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20.

Kuanzia Juni 15 hadi Julai 15, 2022 Shirikisho la Mpira la China liliwateua wachezaji wa kike wenye umri chini ya miaka 20 Mengyao Zou, Xinyue Zhao an Xiaole Liu kushiriki mazoezi ya taifa ya kujiandaa kwa mashindano ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Asia Mwaka 2023.

Kwa maendeleo haya, ni wazi Mkoa wa Shaanxi ambao ni kituo cha Njia ya Hariri na mwendelezaji wa Pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, umejipanga kuwa mfano katika kufikia ustawi wa watu wote na kuchangia busara zake kwa Dunia. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha