

Lugha Nyingine
Miaka mitano baada ya kuzinduliwa kwa Reli ya Mombasa-Nairobi—— njia ya reli inayolinda mazingira ya asili (5)
![]() |
Picha hii iliyopigwa Julai 20 ikionesha Daraja Kuu linalofungwa zana za kuzuia kelele katika Bustani ya Taifa ya Nairobi ya Kenya. (Picha na Kampuni ya uendeshaji wa reli ya Africa Star) |
Reli ya Mombasa-Nairobi iliyozinduliwa rasmi mwaka 2017 inapita Bustani ya Taifa ya Nairobi, na Bustani ya Taifa ya Tsavo ambapo ni eneo la hifadhi za wanyamapori na mimeapori. Ili kupunguza athari kwa mazingira ya asili, hatua nyingi mfululizo zilichukuliwa katika mchakato wa kufanya usanifu na ujenzi wa reli hiyo.
Kwenye msingi wa kufanya utafiti kuhusu tabia za wanyamapori katika maisha yao, na njia ya kuhamahama kwa wanyama pori, wajenzi wa reli walijenga njia 14 na madaraja 79 kwa ajili ya kupita kwa wanyamapori kwenye Reli nzima ya Mombasa-Nairobi. Na kimo cha njia zote za kidaraja ni zaidi ya mita 6.5 ili kuwawezesha wanyama wakubwa kama tembo na twiga kupita. Uzio ulijengwa katika kando mbili za reli hiyo ili kuwazuia wanyamapori kupita na kupunguza uwezekano wa wanyamapori kugongana na treni. Zana za kuzuia kelele zimefungwa kwenye Daraja Kuu katika Bustani ya Taifa ya Nairobi ili kupunguza athari ya treni wakati zinapopita. Wakati wa kufanya usanifu wa reli hiyo, zimechukuliwa hatua mbalimbali kama vile za treni kupita na kuzunguka nje ya eneo la msitu wa mikoko ili kupunguza athari ya reli kwa mikoko na kuulinda msitu wa Mombasa. Hatua hizo zote zinaonesha wazi wajenzi wa mradi wa China wanaheshimu mazingira ya asili, kufuata kanuni za mazingira ya asili, na kulinda mazingira ya asili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma