Kampuni yaanza kuzalisha vidonge vya UVIKO-19 huko Henan, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 04, 2022
Kampuni yaanza kuzalisha vidonge vya UVIKO-19 huko Henan, China
Kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Henan ilianza rasmi kuzalisha vidonge Azvudine, dawa ya kutibu UVIKO-19, huko Pingdingshan, Mkoa wa Henan wa Katikati mwa China, Agosti 2, 2022. (Picha/Chinadaily)

Jumanne wiki hii, kampuni ya teknolojia ya viumbe ya Henan ilianza rasmi kuzalisha vidonge vya kutibu UVIKO-19 Azvudine baada ya kufanya hafla ya uzinduzi mjini Pingdingshan, Mkoa wa Henan wa China. Hii ni hatua muhimu katika mapambano dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona.

Kiwanda cha Pingdingshan cha kampuni hiyo Mei kilipitishwa ukaguzi wa usimamizi wa uzalishaji wa dawa uliofanywa na Idara ya usimamizi ya dawa ya Henan mwezi Mei, kikapata kibali cha kuzalisha vidonge vya aina hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha