Yangling, Silicon Valley ya Kilimo ya China inayoleta Mageuzi kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2022
Yangling, Silicon Valley ya Kilimo ya China inayoleta Mageuzi kwenye “Ukanda Mmoja, Njia Moja”
Mtembeleaji akitazama mfumo wa kiteknolojia na kielelezo cha mradi wa Kampuni ya Teknolojia za hali ya juu za Kilimo ya Shaanxi Xutian, huko Yangling, Mkoa wa Shaanxi nchini China. (Picha na People’s Daily Online)

Eneo la Yangling liko katika Mkoa wa Shaanxi nchini China. Eneo hili kwa sasa limegeuka kuwa la vielelezo vya teknolojia za hali ya juu za kilimo, matumizi ya akili bandia katika kilimo na teknolojia nyingine nyingi ambazo zinaleta mageuzi makubwa kwenye sekta ya kilimo, huku likichangia vilivyo kwenye ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na kuchangia usalama wa chakula duniani. Kutokana na uwepo wa miradi mingi ya kisasa ya teknolojia za hali ya juu katika kilimo, eneo hili limepewa jina la “Silicon Valley ya Kilimo ya China”.

Tarehe 14 Juni, 2019, Rais wa China Xi Jinping alitoa hotuba kwenye mkutano wa 19 wa Baraza la Wakuu wa Nchi Wanachama wa Shirikisho la Ushirikiano la Shanghai (SCO) akisema kwamba "China itaanzisha kituo cha vielelezo vya teknolojia ya kilimo cha SCO na kituo cha vielelezo vya mafunzo cha teknolojia ya kilimo cha SCO katika Mkoa wa Shaanxi, nchini China.

Tangu kutolewa kwa agizo hilo Serikali Kuu ya China na ile ya Mkoa wa Shaanxi zimekuwa zikishirikiana katika kuhakikisha ndoto na maono hayo ya Rais Xi yanatimia na kuzinufaisha nchi husika.

Kwanza lilifunguliwa eneo maalumu la vielelezo la mabadilishano na mafunzo ya teknolojia za kilimo cha SCO hapa Yangling, pia katika eneo hili kumefunguliwa Kituo cha Vielelezo cha Teknolojia za Hali ya Juu za viwanda vya Kilimo cha Yangling.

Miradi hii yote miwili ambayo imeunganishwa kwa ukaribu na kutekelezwa katika eneo moja hilo la Yangling, inatajwa kuwa mahali muhimu pa kuzaliwa ustaarabu wa Kilimo wa China, eneo la kwanza la vielelezo la taifa la teknolojia ya juu ya kilimo la China, mageuzi ya kisasa ya Sayansi na Teknolojia ya Kilimo ya China, eneo la vielelezo kwa kilimo cha kisasa, eneo pekee la biashara huria la China lenye upekee wa kilimo "Ukanda Mmoja, Njia Moja” na Kituo cha Kisasa cha Ushirikiano wa Kimataifa wa Kilimo cha SCO.

Aidha, eneo hili la Yangling kutokana na hamasa ya juu ya kilimo na ukweli kwamba linachukuliwa kama Silicon Valley ya Kilimo ya China, sasa limekuwa na shughuli nyingi za kilimo cha kisasa na chanzo cha teknolojia za hali ya juu katika uboreshaji wa kilimo, uhifadhi wa uoevu wa ardhi na miradi mingine mingi ya mapinduzi ya kilimo.

Ifuatayo ni miradi muhimu inayopatikana kwenye Silicon Valley ya Kilimo ya China:

Eneo Maalumu la Vielelezo la mabadilishano na mafunzo ya teknolojia za kilimo la SCO

Wakati kituo hiki kilipoanzishwa, Vladimir Norov aliyekuwa Katibu Mkuu wa SCO alisema kuwa Kituo cha Kilimo wa SCO kitafanya kazi ya kuhamasisha uvumbuzi wa teknolojia ya kilimo, kubadilishana ujuzi wa hali ya juu na uzoefu, kutatua matatizo katika maendeleo ya kilimo cha kisasa katika nchi za SCO, na kutoa msaada wenye nguvu kwa maendeleo zaidi ya kilimo cha kisasa.

Oktoba 22, 2020, ujenzi wa msingi wa Kituo cha Kilimo cha SCO ulianza rasmi huko Yangling, na kukamilika kwa ujenzi wake sasa kumeleta mabadiliko kutoka kuwa mpango wa upande mmoja hadi kuwa hatua ya pamoja ya nchi wanachama wa SCO. Tarehe 12 Agosti, 2021, Mkutano wa 6 wa Mawaziri wa Kilimo wa SCO ulikagua na kuidhinisha "Ujenzi wa Misingi ya Kilimo ya SCO", na msingi huo ukawa jukwaa la kwanza la kubadilishana kilimo na ushirikiano kwa nchi wanachama wa SCO kujadili, kujenga na kushiriki pamoja.

Kituo cha Vielelezo cha Teknolojia za Hali ya Juu za viwanda vya Kilimo cha Yangling

Yangling ni moja wapo ya mahali palipozaliwa ustaarabu wa kilimo wa China. Historia ya Yangling ni historia ya kilimo cha China na ustaarabu wa sayansi ya kilimo na teknolojia. "Rekodi za Kihistoria za Zhou Benji" inaonesha kuwa zaidi ya miaka 4,000 iliyopita, ofisa wa kwanza wa kilimo katika historia ya China, Houji, "aliagiza watu kulima na kuzalisha nafaka tano" katika eneo hili, na kujenga historia kwa ustaarabu wa kilimo wa China.

Eneo hili limejikita katika maeneo makuu mawili ya kiteknolojia, kwanza ni teknolojia za ufugaji na uzalishaji wa mifugo na teknolojia ya kudhibiti wadudu wanaoshambulia mimea, utafiti na uongezaji wa mboga za majani na matunda.

Tangu kuanzishwa kwa kituo hiki, kimekidhi mahitaji ya China, “uwanja mkuu wa harakati za kilimo kwa maeneo ya vijijini na wakulima", na kimekuwa himaya ya sayansi na teknolojia ya kilimo duniani, ikizingatia mahitaji makubwa ya kimkakati kama vile usalama wa chakula na mahitaji ya chakula ya China. Kimesaidia kuimarisha mageuzi ya mfumo wa kisayansi na elimu, kuamsha vipengele vya ubunifu, na kuhimiza kwa kina uzalishaji, elimu na utafiti.

Mwaka 2016, taasisi ilichukua uongozi katika kuanzisha Muungano wa Uvumbuzi wa Elimu ya Kilimo wa Sayansi na Teknolojia wa Njia ya Hariri, na kuvutia taasisi 95 za sayansi na elimu na makampuni kutoka nchi 18 kujiunga. Miungano mitano ikijumuisha Ubunifu wa Ngano ya Njia ya Hariri na vituo vitatu vya utafiti vya nchi ikijumuisha Kazakhstan vilianzishwa ili kutoa msaada wa kiweledi kwa maendeleo ya kilimo ya kimataifa.

Kampuni ya Teknolojia za Kilimo ya Shaanxi Xutian

Kampuni hii ilianzishwa rasmi katika Eneo la Kielelezo la Yangling, Mkoa wa Shaanxi Machi, 2013. Inachukua mabadiliko ya mitindo ya maisha ya binadamu na kuboresha sifa ya maisha ya watu wa China kama dhamira yake, na inachukua mradi wake wa l-mkulima kama bidhaa yake kuu. Usalama, usafi, afya na lishe ndio dhana kuu, na inajitahidi kujenga mnyororo wa sekta ya kilimo ya teknolojia ya optoelectronic na ujumuishaji wa taa za ukuaji wa mimea, kutumia akili bandia kudhibiti mazingira ya ukuaji wa mimea, na ujumuishaji wa utafiti na maendeleo, uzalishaji na uuzaji wa mimea na vifaa vya kukuza mimea bila kutegemea udongo.

Eneo Lililounganishwa kwa kina la Shaanxi Yangling

Kaulimbiu ya eneo hili la teknolojia za kilimo ni “kuingia kwa kina kwenye muundo mkubwa wa ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” ili kufanya mageuzi kwenye nyanda za tambarare na za juu”.

Uwekezaji katika eneo hili ni karibu Yuan bilioni 4 na limeanzishwa kwa kuzingatia mpangilio wa viwanda wa "maeneo maalumu manne, kituo kimoja na majukwaa matatu". Katika siku zijazo, kitafikia uhusiano usio na kikomo wa Msingi wa Maonyesho ya Teknolojia ya Kilimo ya SCO na Msingi wa Vielelezo vya Mafunzo, na kutekeleza kwa ufanisi "maendeleo kamili ya ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana katika sekta ya kilimo, kujenga “Ukanda Mmoja, Njia Moja", kituo cha kisasa cha ushirikiano wa kimataifa wa kilimo, na kuhimiza msingi wa mabadilishano ya kililmo, maonyesho na mafunzo wa SCO.

Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Xibei Chuo hiki ambacho nacho kiko eneo la Silicon Valley ya Kilimo ya China, Yangling, kilianzishwa Juni, 2010, ni chuo kikuu chenye kujihusisha na taaluma mtambuka, taasisi ya utafiti wa kitaaluma inayojitegemea na jukwaa la utafiti wa kushiriki taaluma nyingi lililoanzishwa na chuo hicho.

Ili kutekeleza kikamilifu manufaa ya jumla ya kilimo cha kuhifadhi maji katika maeneo kame ya Chuo Kikuu cha Kilimo na Misitu cha Xibe, chuo hiki kimefanya mageuzi ya kiubunifu katika mfumo wa usimamizi wa utafiti wa kisayansi, kimeunganisha kwa kiasi kikubwa misingi saba ya utafiti wa kisayansi wa kitaifa na kimkoa katika vyuo vingi, na maeneo kame.

Katika lengo la kuboresha ufanisi wa kina na manufaa ya matumizi ya maji ya kilimo kama msingi, chuo hiki hufanya utafiti wa kimsingi juu ya matumizi ya kilimo chenye kuhifadhi maji, utafiti na maendeleo ya bidhaa za kiufundi, maonyesho na uendelezaji wa utafiti mzima wa uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha