

Lugha Nyingine
Tibet yapata maendeleo katika sekta za afya na elimu
![]() |
Mkazi akisoma kitabu kwenye duka la vitabu huko Lhasa, Mkoa unaojiendesha wa Tibet. (Picha/China Daily) |
Hivi karibuni ofisa mwandamizi wa Mkoa unaojiendesha wa Tibet alisema, katika muongo uliopita mambo ya afya na elimu ya mkoa huo yamepata maendeleo kwa hatua madhubuti.
Mkoa huo unatoa elimu bure ya miaka 15 kwa watoto kutoka chekecheo hadi sekondari ya juu, ambayo ni muda mrefu zaidi kuliko elimu bure ya miaka 9 katika sehemu nyingine za China, alisema Yan Jinhai, mwenyekiti wa serikali ya mkoa huo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika hivi karibuni huko Lhasa, mji mkuu wa mkoa wa Tibet.
Katika muongo uliopita, Tibet pia imesisitiza uboreshaji wa hali ya afya ya wakazi. Wastani wa kadirio la miaka ya kuishi ya wakazi wa huko imezidi miaka 72 kwa hivi sasa. Tangu kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa 18 wa CPC mwezi Novemba, 2012, Tibet imekuwa ikifanya juhudi za kutoa huduma bora ya matibabu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma