Treni za Fuxing “Hulk” zazingatiwa upimaji ili kuhakikisha usalama wa usafiri katika majira ya joto

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2022
Treni za Fuxing “Hulk” zazingatiwa upimaji ili kuhakikisha usalama wa usafiri katika majira ya joto

Agosti 17, wafanyakazi wakipima na kutengeneza magurudumu ya treni za Fuxing (huitwa “Hulk”) ambazo kasi zao ni kilomita 120 kwa saa katika karakana ya Kituo cha Treni cha Magharibi cha Beijing katika Idara ya Treni ya Beijing.

Hiki ndicho kituo pekee cha upimaji na utengenezaji wa "Hulk" katika eneo la Beijing-Tianjin-Hebei, ambacho kinabeba kazi ya kupima na kutengeneza treni 18 zenye mabehewa 261. Kadiri kilele cha kurudi shuleni kwa wanafunzi kinavyowadia, ndivyo wafanyakazi wanavyoharakisha kupima na kutengeneza treni bila mapumziko zaidi ili kuhakikisha usalama wa usafiri. (Mpiga picha:Jia Tianyong/Tovuti ya Chinanews)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha