

Lugha Nyingine
Angola kufanya uchaguzi mkuu leo ambao unaelezwa kuwa wenye ushindani mkubwa (3)
![]() |
Wafuasi wa kisiasa wakiwa mtaani Luanda, Angola, Agosti 22, 2022. (Xinhua/Chen Cheng) |
LUANDA - Takriban wapiga kura milioni 14.3 wa Angola wanatazamiwa kupiga kura leo Jumatano ili kumchagua rais wa nchi hiyo na wajumbe wa Bunge la Taifa.
Wagombea wanane wanaogombea kwa tiketi ya vyama saba vya siasa na mwingine kutoka muungano wa vyama watachuana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, unaoaminika kuwa wenye ushindani mkali tangu uchaguzi wa demokrasia ya vyama vingi uanze nchini humo Mwaka 1992.
Wapiga kura
Angola ilipata uhuru kutoka kwa Ureno Mwaka 1975 baada ya mapambano ya muda mrefu ya kupinga ukoloni. Idadi ya watu wake imeongezeka hadi kufikia watu milioni 32.87 Mwaka 2021. Katiba ya nchi hiyo inaeleza kuwa wapiga kura lazima wawe na umri wa angalau miaka 18.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (CNE), kuna wapiga kura milioni 14.3 waliojiandikisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ambao utajumuisha pia ushiriki wa wapiga kura wa ng’ambo, huku wananchi 22,560 wakitazamiwa kupiga kura kutoka nje ya nchi. Uhusishaji wa haki za kupiga kura kwa watu wanaoishi nje ya nchi, ambao wanapiga kura kwa mara ya kwanza, pia unaleta matarajio ya ushindani mkubwa.
Vyama vinavyoshindana kwenye uchaguzi
Rais hachaguliwi moja kwa moja nchini Angola. Kwa mujibu wa katiba ya Angola, mgombea anayepata kura nyingi kutoka kwenye muungano wa vyama au chama cha kisiasa ambacho kinapata kura nyingi huchaguliwa kuwa rais.
Mwaka huu, vyama saba vya kisiasa na muungano mmoja wa vyama vya kisiasa vinashiriki uchaguzi huo huku vikiwania viti 220 katika Bunge la Taifa. Kati ya viti hivyo 220, 130 huchaguliwa kutoka orodha ya kitaifa ya vyama vya kisiasa, na wabunge 90 waliobaki wanachaguliwa kutoka kwenye orodha ya majimbo, huku kila jimbo kati ya majimbo 18 nchini humo likichagua wabunge watano.
Vyama vinavyoshindana ni Chama tawala cha People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA), the National Union for the Total Independence of Angola (UNITA), National Front for the Liberation of Angola (FNLA), National Patriotic Alliance (APN), the Social Renewal Party (PRS), the Humanist Party of Angola (PHA), the Nationalist Party for Justice in Angola (P-NJANGO), and the Broad Convergence for the Salvation of Angola-Electoral Coalition (CASA-CE).
Uchaguzi huu utakuwa ni wa tano wa aina yake tangu uchaguzi wa demokrasia ya vyama vingi kuanzishwa kwa mara ya kwanza Mwaka 1992 katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika. Chama tawala, People's Movement for the Liberation of Angola (MPLA), kimekuwa kikishinda chaguzi zote zilizofanyika mwaka wa 1992, 2008, 2012 na 2017.
Vinara wa uchaguzi huo
Rais wa sasa Joao Lourenco anagombea kwa tiketi ya chama tawala cha MPLA, kwa matumaini ya kuwania awamu ya pili madarakani. Atakabiliwa na changamoto kutoka kwa mpinzani wake mkuu Adalberto Costa Junior, kiongozi wa chama kikuu cha upinzani UNITA nchini humo.
Katika uchaguzi wa Mwaka 2017, chama tawala cha MPLA kilishinda kwa kura nyingi za asilimia 61, kikifuatiwa na UNITA iliyopata takriban asilimia 27 ya kura zote zilizopigwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma