Mshabiki wa Kungfu aanzisha darasa kwa watoto wa kijijini (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 25, 2022
Mshabiki wa Kungfu aanzisha darasa kwa watoto wa kijijini
Tarehe 16, Agosti, 2022, Liu Yidian, binti wa Liu Long akicheza Kungfu ya China kwenye Kijiji cha Liuzhuang cha Mji wa Pizhou, Mkoa wa Jiangsu, mashariki mwa China.

Liu Long mwenye umri wa miaka 35 ni mshabiki wa Kungfu ya China. Aliona watoto wake watatu pia wamevutiwa na Kungfu na huiga matendo yake wakati alipofanya mazoezi, hivyo alianza kuwaongoza watoto wake kufanya mazoezi pamoja naye, ambapo wanakijiji pia waliwapeleka watoto wao kuja kujifunza kutoka kwa Liu.

Kwa kuwa watoto wanaojifunza Kungfu waliongezeka zaidi, Liu na mkewe walianzisha darasa la Kungfu. Liu anatumai watoto wanaweza kukua kwa furaha na afya njema, na kupenda Kungfu katika maisha yao yote. (Xinhua/Li Bo)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha