

Lugha Nyingine
Timu za Matibabu za kusaidia Hainan zakamilisha kazi kwa mafanikio na kuondoka mfululizo
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 30, 2022
Agosti 29, watu karibu 7000 wa timu za matibabu za kusaidia Hainan kutoka Mikoa ya Fujian, Sichuan, Shandong n.k. waliondoka Haikou kwa mfululizo. Habari zilisema kuwa tangu mwanzo wa mwezi Agosti, maambukizi ya virusi vya korona yalilipuka mkoani Hainan, madaktari na wauguzi zaidi ya elfu 20 waliotoka mikoa na miji zaidi ya 20 nchini walikwenda Mkoa wa Hainan kutoa msaada.
Hivi sasa, hali ya kinga na udhibiti wa maambukizi ya virusi vya korona imekuwa nzuri kwa hatua madhubuti na watu waliothibitishwa kuambukizwa virusi vya korona kwenye jamii wamepungua zaidi. Kuanzia tarehe 26, madaktari wa timu za matibabu za kusaidia Hainan wameanza kuondoka mkoa huo.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma