Barabara mpya ya mwendo kasi ya Xinjiang yahimiza maendeleo ya uchumi ya sifa bora (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 01, 2022
Barabara mpya ya mwendo kasi ya Xinjiang yahimiza maendeleo ya uchumi ya sifa bora
Picha iliyopigwa tarehe 30, Agosti, 2022 ikionesha magari yakipita kituo cha kodi cha barabara ya mwendo kasi ya Yetimbulak-Ruoqiang kwenye Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur, Kaskazini Magharibi mwa China. (Picha/Xinhua)

Barabara mpya ya mwendo kasi inayounganisha Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uyghur wa Kaskazini Magharibi mwa China ilizinduliwa Jumanne ya wiki hii. Barabara hiyo inatazamiwa kuleta urahisi zaidi kwa usafiri wa wakazi wa huko, na kuhimiza maendeleo ya uchumi ya sifa bora katika eneo hilo.

Barabara hiyo ya mwendo kasi yenye urefu wa jumla wa kilomita 300 inaunganisha Tarafa ya Yetimbulak na Wilaya ya Ruoqiang, ikiwa sehemu muhimu ya mtandao wa barabara za mwendo kasi wa China. Barabara hiyo ni barabara ya tatu ya Xinjiang ya kuelekea nje ya nchi, na kasi yake ya kupangwa ni kilomita 120 kwa saa.

Hadi hivi sasa, umbali wa uendeshaji wa magari kwenye barabara za mwendo kasi za Xinjiang umezidi kilomita 7500.

Wilaya ya Ruoqiang inasifiwa kuwa “maskani ya tende ya China”. Hivi sasa matunda hayo yanaweza kuwasilishwa kwenye masoko nje ya Xinjiang kwa muda mfupi zaidi kwa kupitia barabara mpya ya mwendo kasi.

“Tumepata oda kutoka Mji wa Xining, mji mkuu wa Mkoa wa Qinghai wa Kaskazini Magharibi mwa China. Zamani usafiri wa kwenda huko ulichukua saa 7 hivi, lakini kwa kupitia barabara mpya muda huo umefupishwa kuwa nusu yake,” alisema Mehliya Ayup, mpandaji tende wa Wilaya ya Ruoqiang.

Kwa kuwa barabara hiyo inapita eneo la hifadhi ya kitaifa ya Mlima Altun, hivyo yamejengwa madaraja na mahandaki mengi badala ya njia za msingi za jadi.

“Madaraja na mahandaki hayo yamejengwa kwa ajili ya kupunguza athari kwa wanyama pori,” alisema Song Liyan, meneja wa mradi huo wa Kampuni ya Ujenzi wa Mawasiliano ya China. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha