Juhudi za kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi zinaendelea Sichuan, China (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 07, 2022
Juhudi za kutoa misaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi zinaendelea Sichuan, China
Wanakijiji wakiwa wamepanda mtumbwi uliotengenezwa kwa malighafi za mpira wakati wa kuhamishwa kutoka mji mdogo wa Detuo katika Wilaya ya Luding, Mkoa wa Sichuan nchini China, Septemba 6, 2022. (Xinhua/Shen Bohan)

Serikali za Mtaa zimetoa taarifa leo Jumatano kuwa, jumla ya watu 74 hadi sasa wamefariki dunia katika tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 katika kipimo cha Richter lililokumba Wilaya ya Luding, Mkoa wa Sichuan nchini China siku ya Jumatatu.

Makao makuu ya uokoaji yamesema kwenye mkutano na waandishi wa habari leo Jumatano kuwa, katika Tarafa inayojiendesha ya Watibet ya Ganzi hadi kufika Saa 6 mchana leo Jumatano, watu 40 walikuwa wamefariki, 14 walikuwa bado hawajapatikana na 170 wamejeruhiwa, na katika Mji wa Ya'an watu 34 walikuwa wamefariki, 12 walikuwa bado hawajapatikana na 89 wamejeruhiwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha