

Lugha Nyingine
Bustani ya mashamba ya Jasmine ya China kwenye picha zilizopigwa kutoka angani (3)
![]() |
Picha ikionesha njia ya watalii yenye rangi mbalimbali kwenye bustani ya maua ya Jasmine ya China. (Picha/Fu Huazhou) |
Katika majira mapema ya mpukutiko, maua ya Jasmine yanachanua kwenye mashamba makubwa ya bustani ya Jasmine ya China iliyoko Kijiji cha Shijing cha Mji wa Hengzhou wa Mkoa wa Guangxi. Hivi sasa ni majira ya kuchuma maua ya Jasmine, wakulima wa maua wakivaa mavazi ya kuzuia jua kali wanachuma maua ya Jasmine kwa pilikapilika.
“Kila siku ninaweza kuchuma maua ya kilogramu 20 hadi 25, na kila kilogramu yanaweza kuuzwa kwa bei ya Yuan 28-30, hata baadhi ya wakati bei hiyo inafikia Yuan 22.” Mkulima wa maua Lei Shuiping alipanda maua ya Jasmine karibu robo moja ya hekta , na kipato chake cha mwaka kimefikia Yuan 150,000 hadi 20,000 baada ya kuondoa gharama.
Habari zinasema, utoaji wa maua ya Jasmine unachukua asilimia 80 ya utoaji wa ujumla nchini kote China, na asilimia 60 ya duniani kote. Katika miaka ya hivi karibuni, utoaji wa wa maua hayo wa mji wa Hengzhou na sifa zao vinaendelea kupata maendeleo mapya siku hadi siku kwa kutegemea msaada wa teknolojia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma