Kazi ya kuunganisha nyaya za umeme kati ya Baihetan-Zhejiang zinazopitishwa kuvuka Mto Changjiang yakamilika (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2022
Kazi ya kuunganisha nyaya za umeme kati ya Baihetan-Zhejiang zinazopitishwa kuvuka Mto Changjiang yakamilika
Mafundi wakifanya kazi ya kuunganisha nyaya za umeme zinazopitishwa kuvuka Mto Changjiang katika mradi wa kupeleka umeme ya 800kv UHVDC wa Baihetan-Zhejiang (sehemu ya Chongqing) huko Chongqing, Kusini Magharibi mwa China Septemba 13, 2022.

Baada ya kufanya juhudi kwa siku 13, siku hizi kazi ya kuunganisha nyaya zilizopitishwa kuvuka Mto Changjiang katika mradi wa kupeleka umeme wa 800kv UHVDC wa Baihetan-Zhejiang imekamilika. Mradi huo wa kuunganisha nyaya za umeme zenye urefu wa kilomita 2140 ulianzishwa Oktoba, 2021, nyaya hizo zinapita mikoa ya Sichuan, Chongqing, Hubei, Anhui na Zhejiang. Ujenzi wa mradi huo unakadiriwa kukamilika mwishoni mwa Mwezi Septemba, na kuzinduliwa mwezi Novemba mwaka huu. Mradi huo unasifiwa kuwa ni moja ya “Barabara ya mwendo kasi ya umeme ya China”, ukiwa sehemu muhimu ya mradi wa China wa kupeleka umeme wa Mashariki kwa Magharibi. (Xinhua/Huang Wei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha