Mawasiliano kati ya Uganda na China katika sekta ya elimu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 15, 2022
Mawasiliano kati ya Uganda na China katika sekta ya elimu
Jackie Kazalwa, mwalimu wa Shule ya Msingi ya Mfano ya Entebbe-Changsha, akionyesha baadhi ya kazi zilizofanywa na wanafunzi katika darasa la sanaa huko Entebbe, Uganda, Septemba 7, 2022. (Picha na Nicholas Kajoba/Xinhua)

Shule ya Msingi ya Mfano ya Entebbe-Changsha ilianzishwa kwa msingi wa maendeleo ya watoto na vijana kwenye ufundi wa kazi ya kusoma masomo ya kawaida ya kupita kiasi katika shule. Shule hiyo ilijengwa kwa msaada wa Serikali ya mji wa Changsha, China. Kutokana na ombi la Entebbe, Mji wa Changsha ulitoa misaada kwa mradi wa ukarabati wa shule hiyo Mwaka 2019.

"Shule hiyo inasaidia wasichana na wavulana wa Uganda ili waweze kupata elimu na ufundi wa kazi unaohitajika hivi leo," Robinah Nakamya, mkuu wa shule hiyo, aliwaambia waandishi wa habari wa Xinhua katika mahojiano ya hivi majuzi.

Nakamya alisema ufundi wa kazi ulihusisha sanaa, usanifu, kompyuta, uchumi wa nyumbani na michezo.

Pia alisema kwamba baada ya ukarabati kufanyika mwaka 2019, idadi ya wanafunzi iliongezeka hadi 850, na kulikuwa na wanafunzi 250 hapo kabla.

John Bosco Izachary, mzazi wa watoto watatu ambao wanasoma katika shule hiyo, aliwaambia waandishi wa habari wa Xinhua kwamba alichagua shule hiyo kwa kuwa kiwango cha mafunzo ya shule hiyo kimeinuliwa.

Shule hiyo ni moja ya mafanikio mengi yaliyopatikana katika maendeleo ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Uganda katika miongo kadhaa iliyopita. Na mwezi ujao nchi hizo mbili zitaadhimisha miaka 60 ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia.

Mbali na kutoa msaada kwa shule ya msingi, China inaendeleza kwa kina ushirikiano na Uganda katika nyanja tofauti za elimu na ufundi wa kazi.

Chuo Kikuu cha Makerere, ambacho ni chuo kikuu cha kiwango cha juu nchini Uganda kilianzisha Chuo cha Confucius. Hivi sasa, chuo hicho kinatoa mafunzo ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wake na wa nje ya chuo.

Chuo hicho cha Confucius pia kinatoa mafunzo ya Lugha ya Kichina kwa waalimu wa Lugha ya Kiuganda. Kutokana na juhudi hizo, Uganda imeweka somo la Lugha ya Kichina kwenye masomo ya shule za sekondari.

Katika Chuo Kikuu cha Makerere, kuna " mdhamini wa masomo wa urafiki mkubwa kutoka Balozi wa China" unaofadhiliwa na Ubalozi wa China nchini Uganda, ambao unatolewa kwa wanafunzi wenye matatizo ya kiuchumi ambao ni wanafunzi bora katika masomo na wanaofuata maadili. Katika miaka mitano iliyopita, wanafunzi 100 hivi wamepata uungaji mkono wa kifedha kwa mdhamini wa masomo wa balozi wa China na kutimiza ndoto zao.

Mwaka 2020, China ilianzisha Karakana ya Luban ya kutoa mafunzo ya kiwango cha juu ya ufundi wa kazi ili kuwasaidia vijana wanaokidhi mahitaji ya soko la ajira.

China pia imetoa msaada wa dola milioni 30 za kimarekani kwa ajili ya ujenzi wa chuo cha mafunzo ya ufundi wa kazi. Uganda inaona Chuo cha Namanve katika Taasisi ya Utafiti wa Viwanda ya Uganda kimefanya kazi muhimu katika kuwaandaa vijana wenye ufundi wa kazi wakati nchi hiyo inapotafuta ongezeko la uchumi unaoongozwa na sekta ya viwanda. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha