China yakumbuka Vita vya kupambana na uvamizi wa Japan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 19, 2022
China yakumbuka Vita vya kupambana na uvamizi wa Japan
Tarehe 18, Septemba, 2022, Watu wakipiga kengele kubwa kwenye hafla ya kukumbuka tukio la Septemba 18 na Vita vya Watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Jeshi la Japan kwenye jumba la makumbusho ya historia ya tukio la Septemba 18 huko Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning wa Kaskazini Mashariki mwa China. (Xinhua/Yang Qing)

Jumapili ya wiki iliyopita milio ya honi ya tahadhari ya kuhuzunisha ilisikika Shenyang, Mji Mkuu wa Mkoa wa Liaoning wa Kaskazini Mashariki mwa China, ambapo madereva wa magari barabarani pia walipiga honi, siku hiyo ni ya miaka 91 ya tukio la Septemba 18, ambayo ni alama ya kuanzishwa kwa uvamizi wa Japan dhidi ya China.

Kuanzia mwaka 1995, kila ifikapo siku hiyo, mlio wa honi wa tahadhari ya shambulizi kutoka angani unasikika mjini Shenyang, mji huo umekumbuka tukio la Septemba 18 kwa miaka 28 mfululizo.

Katika Jumba la Makumbusho ya Historia ya Septemba 18, watu wa sekta mbalimbali walikusanyika pamoja siku hiyo, wakishiriki kwenye hafla ya kukumbuka tukio la Septemba 18 na vita vya watu wa China vya kupambana na uvamizi wa Japan.

Saa 3 na dakika 18 hivi asubuhi, wajumbe 14 wa sekta mbalimbali wakilindwa na kikosi cha bendera cha Jeshi la Ukombozi wa Umma la China, walipiga kengele kubwa kwa mara 14, kwa kukumbuka vita vya kupambana na uvambizi wa jeshi la Japan vilivyofanyika kwa miaka 14.

Tarehe 18, Septemba, 1931, Jeshi la uvamizi la Japan lilibomoa sehemu moja ya reli iliyodhibitiwa nalo, likalaumu Jeshi la China kuharibu reli na kuanzisha shambulizi kwa kisingizio hicho. Baadaye ya siku hiyo walipiga mabomu dhidi ya kambi za kijeshi karibu na Shenyang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha