Shule za Wapalestine za Jerusalem zafungwa ili kupinga Israel kuzilazimisha kupokea vitabu vyake vya masomo (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 20, 2022
Shule za Wapalestine za Jerusalem zafungwa ili kupinga Israel kuzilazimisha kupokea vitabu vyake vya masomo
Picha iliyopigwa tarehe 19, Septemba ikionesha uwanja wa michezo usiokuwepo kwa wanafunzi katika shule ya Wapalestine karibu na Silwan, Jerusalem Mashariki. (Picha ilipigwa na Muammar Awad/Xinhua)

Shule 150 hivi za Wapalestine katika Jerusalem Mashariki zilifungwa Jumatatu ya wiki hii, ili kupinga serikali ya Israel kujaribu kukagua vitabu vyao vya masomo na kuzilazimisha kupokea masomo ya Israel.

Shirika la habari la serikali ya Palestine WAFA liliripoti kuwa, takriban wanafunzi 100,000 hawaendi shuleni kwa sababu ya mgomo wa masomo, hiki ni kitendo cha kuonya baada ya serikali ya Israel kuanza kuchukua hatua ya kuadhibu shule ili kuzilazimisha “kuondoa masimulizi ya Wapalestine kutoka kwenye masomo, na kuweka masimulizi ya Waisrael tu”.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha