Mtu aliyekwama milimani wakati wa tetemeko la ardhi la Sichuan aliokolewa baada ya siku 17

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2022
Mtu aliyekwama milimani wakati wa tetemeko la ardhi la Sichuan aliokolewa baada ya siku 17
Tarehe 21, Septemba, 2022, helikopta iliyombeba Gan Yu (kwenye kiti cha nyuma, kulia) ikiwasilia Wilaya ya Luding, Mkoa wa Sichuan wa Kusini Magharibi mwa China.

Mfanyakazi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa maji cha China aligunduliwa bado kuwa na uhai baada ya kukwama milimani kwa siku 17 wakati wa tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.8 kwenye kipimo cha Richter kutokea katika Mkoa wa Sichuan, China.

Jumatano ya wiki hii, Gan Yu, mfanyakazi mwenye umri wa miaka 28 wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya maji cha Wilaya ya Luding ya Mkoa wa Sichuan, aliokolewa na mwanakijiji wa huko. Hivi sasa anatibiwa kwenye Hospitali ya Huaxi ya Chuo Kikuu cha Sichuan.

Video iliyotangazwa na televisheni ya taifa ya China CCTV inaonesha kuwa, Ni Taigao, ambaye ni mwanakijiji aliyegundua Gan, aliamua kushiriki kwenye shughuli ya kumtafuta Gan kwa sababu anajua zaidi hali ya milimani huko.

Habari za CCTV zilisema, asubuhi ya Jumatano ya wiki hii, Bw. Ni alisikia sauti ya mtu aliyepiga kelele ya kuomba msaada, akagundua Gan aliyelala chini kwenye msitu.

Gan alimwambia Ni kuwa, alinusurika kwa kutegemea kula matunda pori na kunywa maji ya chemchemi mlimani.

Naibu mkuu wa hospitali Wu Hong alisema, sehemu nyingi za mwili wa Gan zimejeruhiwa, mifupa yake kadhaa zimevunjika, na pia ameambukizwa vibaya na vijidudumaradhi.

Madaktari walisema, ingawa hivi sasa Gan anaonekana ni mdhaifu, lakini dalili muhimu za afya yake ni tulivu.

Wakati tetemeko la ardhi lilipotokea Luding tarehe 5, Septemba, Gan na mwenzake waliacha fursa ya kukimbia, badala yake walibaki kazini kwenye kituo cha uzalishaji wa umeme, na kujitahidi kuzuia mafuriko ya maji kuharibu vijiji vya chini. Mwenzake aliokolewa tarehe 8, Septemba.

Hadi tarehe 11, Septemba, tetemeko hilo la ardhi limesababisha vifo vya watu 93.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha