Mafunzo ya kutengeneza kahawa yawasaidia walemavu wa masikio wapate ajira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 26, 2022
Mafunzo ya kutengeneza kahawa yawasaidia walemavu wa masikio wapate ajira
Mwalimu wa lugha ya ishara ya mikono Qu Wenmin (kulia wa juu) akitafsiri masomo kwa wanafunzi wenye ulemavu wa masikio kwenye darasa bure la “mtengenezaji mkimya wa kahawa” tarehe 22, Septemba.

Jumapili ya nne ya mwezi Septemba kila mwaka ni Siku ya Walemavu wa Masikio Duniani. Kuanzia mwaka 2019, Shule ya Uchumi wa Mji ya Shaanxi imekuwa ikitoa mafunzo bure ya mtengenezaji wa kahawa kwa walemavu wa masikio. Wanafunzi wanaweza kujifunza ufundi wa kutengeneza kahawa na kupata ujuzi wa kuendesha mkahawa, ili kuwasaidia kuweka msingi wa kuanzisha biashara ya kahawa au kuingia kwenye sekta hiyo. Hadi hivi sasa, tayari wapo wahitimu zaidi ya 20 wanaoajiriwa kwenye mikahawa ya sehemeu mbalimbali humu China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha