Kuachia kuvuka mto kwa kuteleza kwenye kamba za chuma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 27, 2022
Kuachia kuvuka mto kwa kuteleza kwenye kamba za chuma
Picha iliyopigwa tarehe 14, Septemba ikionesha bonde la Mto wa Nu lililoko Yunnan, China. (Picha/Xinhua)

“Kuteleza kwenye kamba za chuma” kulikuwa njia muhimu ya kuvuka mto ili kwenda nje kwa watu wanaoishi kwenye kando mbili za Mto Nujiang katika jimbo linalojiendesha la kabila la Walisu la Nujiang, Kaskazini Magharibi mwa Mkoa wa Yunnan, China. Mnamo mwaka 2013, wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya China na ofisi ya kuondoa umaskini ya baraza la serikali la China zilifanya utafiti kuhusu hali ya kuvuta mto kutegemea kuteleza kwenye kamba za chuma nchini kote China, vikaamua kutekeleza mradi wa “kubadilisha kamba hizo kuwa madaraja”, ili kuwasaidia watu wa eneo la milima kukomesha zama za kuvuta mto kwa kutegemea kuteleza kwenye kamba za chuma.

Kutokana na mradi huo, kamba 42 zilizokuwepo juu ya Mto Nujiang zilibadilishwa kuwa madaraja 36 ya kuvuka mto, ambayo yametimiza matarajio ya watu wanaoishi kwenye kando mbili za Mto Nujiang.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha