Waziri Mkuu Li asema China itatoa mazingira rahisi kwa vipaji kutoka nje (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 01, 2022
Waziri Mkuu Li asema China itatoa mazingira rahisi kwa vipaji kutoka nje
Waziri Mkuu wa China Li Keqiang akiwa katika picha ya pamoja na wataalam kutoka nje ya China ambao wamepokea tuzo ya Urafiki Mwaka 2022, inayotolewa kila mwaka na Serikali ya China kwa ajili ya kuwaenzi wataalam bora wa kigeni nchini China, kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing, Mji Mkuu wa China, Septemba 30, 2022. (Xinhua/Yin Bogu)

BEIJING - China itatoa mazingira rahisi na huduma bora kwa vipaji vya kigeni kufanya kazi nchini China na kutoa msaada zaidi kwa mazingira yao ya utafiti na jukwaa la uvumbuzi, Waziri Mkuu wa China Li Keqiang amesema Ijumaa wiki hii.

Li ameyasema hayo kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijingg alipokutana na wataalamu wa kigeni waliopata tuzo ya Urafiki Mwaka 2022, inayotolewa kila mwaka na Serikali ya China kwa ajili ya kuwaenzi wataalam bora wa kigeni nchini China.

Amepongeza mchango unaotolewa na wataalamu hao wa kigeni katika mageuzi, ufunguaji mlango na mabadilishano kati ya China na nchi za nje.

Li amebainisha kuwa China bado ni nchi kubwa zaidi inayoendelea duniani, na ujenzi wa usasa unabaki kuwa kazi ya muda mrefu na ngumu. Amesema haijalishi hali ya kimataifa inaweza kubadilika vipi, China itajikita katika kuendesha mambo yake vizuri na kuhakikisha maisha mazuri kwa watu wa China.

Mwaka huu, kutokana na athari za mambo yasiyotarajiwa, uchumi wa China umekabiliwa na shinikizo jipya la kushuka, lakini kwa ujumla, umeonyesha ahueni ya kawaida, Li amesema.

"Tuna imani na uwezo wa kuuweka uchumi kukua na kujiendesha ndani ya viwango vivyofaa na kukuza maendeleo endelevu na ya kiuchumi," ameongeza.

Huku akieleza kwamba China ina deni la maendeleo yake ya haraka kwa mageuzi na ufunguaji mlango, Li amesema China itaendelea kuimarisha mageuzi, kufungua mlango zaidi, na kutia msukumo mkubwa katika ukuaji wa uchumi.

"Tutaendelea kuimarisha mageuzi ya kugatua mamlaka, kurahisisha utawala na kuboresha huduma za serikali, kuchukulia aina zote za wadau wa soko kwa usawa, na kuhimiza mazingira ya biashara ya kimataifa yenye mwelekeo wa soko na sheria," Li amesema.

Ameongeza kuwa, China itahimiza ushirikiano wa kimataifa katika uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia kwa mtazamo wenye uwazi zaidi na kuhimiza mafanikio ya uvumbuzi ili kunufaisha Dunia.

Akibainisha kuwa wataalam wa kigeni ni wajumbe wa urafiki na uhusiano muhimu kati ya China na Dunia, Li amesema China inakaribisha wataalam wa kigeni kushiriki katika mradi wa usasa wa China kwa njia mbalimbali.

Washindi hao wa Tuzo ya Urafiki ya China wamemshukuru Li na Serikali ya China na kueleza nia ya kuendelea kuchangia maendeleo na mabadilishano kati ya China na Dunia.

Kwa mwaliko wa Li, wataalamu hao wa kigeni baadaye walihudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 73 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Manaibu Waziri Wakuu Han Zheng na Liu He.

Mwaka huu, wataalam 49 wa kigeni kutoka nchi 21 wamepokea tuzo hiyo.

Tuzo ya Urafiki ya China ni tuzo ya juu zaidi ya kuwapongeza wataalam wa kigeni ambao wametoa mchango bora kwa harakati za usasa za China. Tangu kuanzishwa kwake Mwaka 1991, jumla ya wataalam wa kigeni 1,848 wamepokea tuzo hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha