Aliyekuwa mvuvi aongoza kijiji kuelekea ustawi (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2022
Aliyekuwa mvuvi aongoza kijiji kuelekea ustawi
Wang Shumao (katikati) akijadiliana na wenzake ofisini kwenye Kijiji cha Tanmen cha Mkoa wa Hainan, Kusini Mwa China tarehe 14, Septemba, 2022. (Xinhua/Yang Guanyu)

Wang Shumao, ambaye ni mwanakijiji wa Mkoa wa Hainan wa Kusini mwa China, alipokuwa na umri wa miaka 18 tayari alikuwa mvuvi mwenye uzoefu, lakini wakati huo hakutegemea atakuwa kiongozi wa kijiji baada ya miaka kadhaa.

Wang alizaliwa mwaka 1956 katika Kijiji cha Tanmen cha Mashariki mwa Mkoa wa Hainan. Alikuwa anasafiri na kuvua samaki kwenye Bahari ya Kusini katika muda mkubwa wa maisha yake.

Katika miaka mingi iliyopita, aliwahi kuwa nahodha wa meli yake mwenyewe, alikuwa mwalimu wa vijana wa kijiji chake, alikuwa katibu wa tawi la chama la kijiji ambapo aliwaongoza wanakijiji kuendeleza shughuli za uvuvi na utalii ili wanakijiji waongeze mapato na kuishi maisha mazuri.

Mwanafunzi wake Chen Zebo akikumbuka alisema, “nilipokuwa na umri wa miaka 13, kijiji chetu kilikuwa na umaskini sana, ambapo nilikuwa sina ujuzi hata kidogo juu ya kuvua samaki, lakini mwalimu Wang alinifundisha bila ya kuficha, kweli anawafuatilia sana wanakijiji wenzake."

Chini ya uongozi na msaada wake, wavuvi zaidi ya 40 wa kijiji hicho walianzisha vituo 33 vya kufuga samaki, na shughuli zao za utalii pia zimeendelezwa vizuri.

Wang amechaguliwa kuwa mjumbe wa Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) mwaka huu. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha