Serikali ya Ufaransa yatangaza mpango wa kubana matumizi ya nishati ili kukabiliana na msukosuko wa nishati

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 08, 2022
Serikali ya Ufaransa yatangaza mpango wa kubana matumizi ya nishati ili kukabiliana na msukosuko wa nishati
Oktoba 6, katika Mji wa Lille, kaskazini mwa Ufaransa, mkazi mmoja anajaza mafuta kwenye kituo cha mafuta cha Supamaketi ya Auchan. Siku hizi, vituo vingi vya mafuta vinavyomilikiwa na Kundi la Total Group la Ufaransa vilifungwa kwa muda kutokana na kukatizwa kwa utoaji wa mafuta, na kusababisha foleni ndefu katika vituo vingine vya mafuta.

Ili kukabiliana na msukosuko wa nishati unaozidi kuwa mbaya siku hadi siku, serikali ya Ufaransa ilianza kutekeleza mpango wa taifa wa kubana matumizi ya nishati Tarehe 6, ikitoa wito wa kuwataka watu wa nchi nzima wafanye juhudi ili kuepusha hatari ya kusitishwa kwa utoaji wa nishati wakati wa majira ya baridi.

(Shirika la Habari la China,Xinhua/Mpiga picha:Sebastian Kurgi )

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha