Rais Xi Jinping asisitiza kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa CPC katika vikosi vya jeshi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 25, 2022
Rais Xi Jinping asisitiza kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa CPC katika vikosi vya jeshi
Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihudhuria mkutano wa maofisa viongozi wa kijeshi na kutoa hotuba muhimu hapa Beijing, China, Oktoba 24. 2022. (Xinhua/Li Genge)

BEIJING - Xi Jinping, Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu aliagiza vikosi vya kijeshi vya China kusoma, kueneza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC, na kujitahidi kufikia lengo lililowekwa la miaka 100 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma (PLA).

Xi, ambaye pia ni Rais wa China na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC), ameyasema hayo alipohudhuria kwenye mkutano wa maofisa viongozi wa kijeshi.

Zhang Youxia na He Weidong, ambao ni wajumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC na manaibu wenyeviti wa CMC, pamoja na Xu Qiliang, walihudhuria na kuhutubia mkutano huo.

Xi amesema, katika miaka mitano isiyo ya kawaida na ya kipekee tangu Mkutano Mkuu wa 19 wa CPC Mwaka 2017, CMC imeongoza vikosi vya jeshi kupata maendeleo makubwa na kuleta mabadiliko makubwa katika ulinzi wa kitaifa na kijeshi.

“CMC imeshikilia uongozi kamili wa Chama juu ya vikosi vya jeshi la ukombozi wa umma, kudumisha na kupanua maendeleo ya haraka na mazuri katika ujenzi wa jeshi lenye nguvu, na kuleta usasa wa kijeshi na uwezo wa kupambana kwa kiwango cha juu,” amesema.

Xi ameeleza kuwa, Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC uliohitimishwa hivi karibuni una umuhimu mkubwa kwa azma ya China kujenga nchi ya kijamaa yenye maendeleo ya kisasa katika sekta zote na kuendeleza ustawi wa Taifa la China katika nyanja zote. Pia ni muhimu katika kutimiza lengo lililowekwa kwa ajili ya miaka 100 tangu kuanzishwa PLA na kujenga vikosi vya kijeshi kuwa vyenye hadhi ya kimataifa.

“Itakuwa kazi muhimu zaidi ya kisiasa kwa Chama kizima, nchi na vikosi vya jeshi kusoma, kueneza na kutekeleza kanuni elekezi za Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC” amesema.

Kabla ya mkutano huo, Xi alikutana na wajumbe, hususani wajumbe maalumu waalikwa na washiriki wasiopiga kura wa PLA na vikosi vya polisi waliokuwepo kwenye Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC na alipiga picha ya pamoja nao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha