Ufundi wa China wasaidia Burundi kuongeza utoaji wa mpunga (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2022
Ufundi wa China wasaidia Burundi kuongeza utoaji wa mpunga
Oktoba 29, wakulima wakipanda mimea ya Mpunga Chotara katika Wilaya ya Kihangga, Mkoa wa Bubanza, Burundi.

Katika miaka mingi iliyopita, China imepeleka wataalam wa kilimo kwenda sehemu mbalimbali za Burundi, ambapo wakitegemea Kituo cha vielelezo vya Ufundi wa Kilimo cha China nchini Burundi kutoa mafunzo ya ufundi wa kilimo kwa wakulima wa mikoa 14 na vijiji 22 vilivyopanda mpunga. Mtaalamu wa kilimo wa China nchini Burundi Yang Huade alisema kuwa timu ya wataalam ilifanikiwa kuongeza utoaji wa mpunga kutoka tani 3 hadi tani 10 kwa kila hekta kwa wastani, kutimiza ongezeko kubwa la kasi sana, na kutoa mchango kwa usalama wa nafaka za nchi hiyo.

(Mpiga picha: Dong Jianghui/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha