Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-14 waingia kwenye moduli ya maabara ya Mengtian (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 04, 2022
Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-14 waingia kwenye moduli ya maabara ya Mengtian
Picha hii ya skrini iliyopigwa katika Kituo cha Udhibiti wa Safari ya Anga ya Juu cha Beijing Novemba 3, 2022 ikionyesha hatch ikifunguliwa kwenye moduli ya maabara ya Mengtian. (Picha na Sun Fengxiao/Xinhua)

BEIJING - Wanaanga wa China kwenye Chombo cha Shenzhou-14 wameingia kwa mafanikio katika moduli ya maabara ya Mengtian ya kituo cha anga ya juu cha China cha Tiangong saa 9:12 alasiri (Saa za Beijing) siku ya Alhamisi, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.

Katika mwendelezo, wanaanga hao kwenye chombo cha Shenzhou-14 katika kituo hicho cha anga ya juu watakaribisha kuwasili kwa chombo cha mizigo cha Tianzhou-5 na chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15, shirika hilo limesema.

Wanaanga kwenye chombo cha Shenzhou-14 na Shenzhou-15 watafanya mzunguko wa pamoja katika obiti kwa mara ya kwanza katika historia ya anga ya juu ya China.

China ilirusha moduli ya maabara ya anga ya juu ya Mengtian Tarehe 31 Oktoba mwaka huu, na kufikisha ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China katika hatua ya mwisho. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha