

Lugha Nyingine
Abiria Mchina aliyeokoa mtoto mdogo kwenye ajali ya ndege ya Ziwa Viktoria asifiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania (2)
![]() |
Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa akienda hospitali kumtembelea Zhang Lin. Picha ilitolewa na mhojiwa. |
Abiria mmoja wa China kwenye ndege ya Tanzani iliyopata ajali aliokoa kijasiri mtoto mdogo baada ya ndege kuanguka kwenye Ziwa Vikotoria, alipata shukuru na kusifiwa na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.
Abiria huyo wa China anaitwa Zhang Lin, ambaye ni kiongozi wa idara ya uhandisi ya tawi la Tanzania la kampuni ya pili ya barabara ya mwendokasi ya CCCC, kampuni ya ujenzi inayomilikiwa na serikali ya China. Zhang Lin alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Global Times tarehe 8 alieleza mambo yote.
“Wakati huo nilikuwa nikikaa kwenye kiti cha safu ya pili ndani ya ndege, ambapo maji yalianza kuingia kwenye sehemu ya abiria ya mbele. Abiria wengi walishtuka na kuhangaika sana, wakaanza kuomba Mungu ,” alisema Bw. Zhang, na aliongeza kuwa, kwanza alivaa mavazi ya uokozi, akawasaidia wahudumu wa ndege kufungua mlango wa dharura kwa abiria wengine.
Baada ya kutoka chombo kwa kuogelea, Bw.Zhang alipanda ubawa wa ndege unaoelea, akisaidia kuongoza wengine kujiokoa.
Bw.Zhang alisema, aliona mlangoni mwa sehemu ya abiria mtu mmoja aliyebeba mtoto alijitahidi sana kutoka, mara alielekea kwake na kumbeba mtoto.
“Wakati huo hali ilikuwa ya hatari sana, sikuweza kufikiria chochote kingine ila kumwokoa kwa haraka,” alisema Bw.Zhang.
Baada ya ndege kuanguka ziwani, wavuvi waliokuwapo karibu mara waliendesha meli ndogo kuelekea sehemu ya ajali kufanya uokozi, ambapo Bw.Zhang na watu wengine waliokolewa. Baada ya kufika kandoni, Bw.Zhang aliwakabidhi madaktari mtoto huyo, na walilazwa hospitalini kutibiwa zaidi.
Bw.Zhang alimwambia mwandishi wa habari wa Global Times kuwa, mama wa mtoto aliyeokolewa Jumatatu alikuja kwenye hospitali kumwangalia na kumshukuru. “Wewe uliokoa maisha ya mtoto wangu, bila ya msaada wako, mambo yatakuwa mabaya yasiyofikirika ,” alisema huyu mama.
Baada ya kuchunguzwa na kufanya upimaji wa afya katika hospitali, Bw.Zhang amekuwa na hali nzuri ya afya licha ya kujehuriwa kidogo kwenye miguu. Hivi sasa ameondoka hospitali na amerudi kazini.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma