Eneo la Teknolojia la Huawei lasaidia kuhimiza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Angola

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 16, 2022
Eneo la Teknolojia la Huawei lasaidia kuhimiza sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano nchini Angola
Tarehe 14 Novemba, 2022, mfanyakazi kutoka Angola wa Kampuni ya Huawei (Kulia) akionesha bidhaa kwa mtembeleaji katika hafla ya uzinduzi wa Eneo la Teknolojia la Huawei la Angola, huko Luanda, Angola. (Mpiga picha: Lyu Chengcheng/ Shirika la Habari la China, Xinhua)

Kampuni ya Huawei ya China imeanzisha eneo la teknolojia nchini Angola ambalo linatarajiwa kusaidia kuwaandaa wataalamu zaidi wenyeji katika sekta ya teknolojia ya habari na mawasiliano (ICT) na kuharakisha mchakato wa kidijitali katika nchi hii ya kusini mwa Afrika.

Katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika Jumatatu, Kampuni ya Huawei na Wizara ya Mawasiliano ya posta, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Jamii ya nchi hiyo zimetia saini makubaliano ya maelewano (MoU) huko Luanda, Angola, kwamba kampuni ya Huawei itasaidia nchi hiyo kuwaandaa wataalamu wenyeji zaidi ya 10,000 za sekta ya TEHAMA katika miaka mitano ijayo.

Kampuni ya Huawei ilisema mbali na ufadhili wa masomo kwa wanafunzi, maprofesa na taasisi hodari, pia itafanya vitabu vya masomo vitumike hadharani kwa taasisi za elimu za huko.

Waziri wa Mawasiliano, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ya Jamii, Mario Oliveira, alisema katika hafla hiyo kwamba eneo hilo litahimiza maendeleo ya teknolojia ya nchi hiyo, na kutoa mafunzo sanifu kwa vigezo vya kimataifa kwa mafundi wa Angola na wa nchi nyingine za Afrika.

Balozi wa China nchini Angola, Gong Tao alisema, China itasaidia Angola kuendeleza uchumi wa kidijitali, akiongeza kuwa mradi huo utahimiza mageuzi ya kidijitali ya Angola na maendeleo ya uvumbuzi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha