Msichana aliyekatwa mguu katika tetemeko la ardhi awa hodari wa kuteleza ubao kwa mguu bandia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2022
Msichana aliyekatwa mguu katika tetemeko la ardhi awa  hodari wa kuteleza ubao kwa mguu bandia

Tarehe 15, Novemba, ingawa hali ya hewa ilikuwa baridi mjini Chengdu, Mkoa wa Sichuan, China, baadhi ya wapenda michezo walikwenda bustani kufanya michezo, akiwemo Hu Yue, msichana mwenye umri wa miaka 26. Wakati tetemeko la ardhi lilipotokea Wenchuan mkoani Sichuan mwaka 2008, Hu Yue aliyekuwa na umri wa miaka 12 alikwama chini ya majengo yaliyoanguka, baada ya kuokolewa alilazwa hospitali na kukatwa mguu wake wa kushoto. Lakini mwaka mzima baadaye , msichana huyo mwenye matumaini alitambua mchezo anaopenda zaidi, yaani kuteleza kwa ubao.

Kwa kuwa kufanya mchezo wa kuteleza kwa ubao kunahitaji nguvu ya miguu miwili, Hu Yue anayetegemea mguu mmoja anakabiliwa na ukomo zaidi na changamoto zaidi. Baada ya kufanya juhudi za zaidi ya miaka kumi, Hu Yue amezoea vizuri mguu wake bandia wa chuma, na kuwa hodari wa kuteleza kwa ubao. Hata alishiriki kwenye ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya majira ya baridi ya Beijing 2022. (Picha zilipigwa na Zhang Lang/China News)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha