Marekani yazindua safari ya mwezini ya Artemis I

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 17, 2022
Marekani yazindua safari ya mwezini ya Artemis I
Roketi ya Shirika la Anga la Marekani (NASA) ya Mfumo wa Urushaji vyombo kwenye anga ya juu iliyobeba chombo cha Orion ikirusha chombo cha majaribio cha Artemis I katika Kituo cha Anga ya juu cha NASA cha Kennedy huko Florida, Marekani, Novemba 16, 2022. NASA imezindua safari ya mwezini ya Artemis I Jumatano baada ya majaribio mawili yaliyoshindwa, na kutuma roketi kubwa ya mwezini ya shirika hilo na chombo kilichounganishwa cha Orion kwenye safari ya kuzunguka mwezi. (Keegan Barber/NASA/kutumwa kupitia Xinhua)

LOS ANGELES – Shirika la Anga ya juu la Marekani (NASA) Jumatano limezindua safari ya mwezini ya Artemis I baada ya majaribio mawili yaliyoshindwa, na kutuma roketi kubwa ya mwezini ya shirika hilo na chombo kilichounganishwa cha Orion kwenye safari ya kuzunguka mwezi.

Roketi ya Mfumo wa Urushaji vyombo kwenye anga ya juu (SLS) na chombo cha anga ya juu cha Orion vilipaa juu Jumatano saa 7:47 usiku kwa Saa za Kawaida za Mashariki (0647 GMT) kutoka Kituo cha Anga ya juu cha NASA cha Kennedy huko Florida, Marekani.

Kufuatia uzinduzi huo, NASA ilithibitisha kujitenga kwa roketi dhabiti. Mfumo wa uwasilishaji wa moduli ya huduma na mfumo wa urushaji vyombo imefaulu kutenganishwa na chombo cha anga cha Orion.

Hatua kuu ya kukata injini ya SLS ilikuwa imekamilika. Hatua ya msingi imetenganishwa na hatua ya muda ya kusukuma mgandamizo wa hali ya baridi na chombo cha anga cha Orion. Baadaye safu za jua za Orion zilikamilisha kufungwa.

Katika muda wote wa misheni hiyo ya siku 25, chombo cha anga ya juu cha Orion kitasafiri maili 280,000 (kilomita 450,000) kutoka dunia na maili 40,000 kutoka upande wa mbali wa mwezi, kwa mujibu wa NASA.

NASA imesema, chombo cha Orion kitakaa angani kwa muda mrefu zaidi kuliko chombo chochote cha anga cha binadamu bila kutia nanga kwenye kituo cha angani na kurudi dunia haraka na kikiwa na joto zaidi kuliko hapo awali.

Chombo hicho kimepangwa kurejea duniani mnamo Desemba 11 na kutua kwenye pwani ya San Diego, California.

Ni jaribio la tatu la uzinduzi wa misheni ya mwezi ya Artemis I baada ya NASA kufuta jaribio lake la kwanza la uzinduzi la Agosti 29 kutokana na tatizo la injini kuvuja na baadaye kusitisha jaribio lake la pili la uzinduzi Septemba 3 kutokana na tatizo la kuvuja.

Jaribio la safari ya anga ya juu ya Artemis I ni misheni isiyo na wanaanga kuzunguka mwezi ambayo itafungua njia kwa ajili ya majaribio ya chombo chenye wanaanga na uchunguzi wa siku zijazo wa mwezi ikiwa ni sehemu ya mpango wa NASA wa Artemis.

Kwa mujibu wa NASA, malengo ya msingi ya Artemis I ni kuonyesha mifumo ya Orion katika mazingira ya anga na kuhakikisha usalama wa wanaanga kuingia tena, kushuka, kutua duniani na kupata utimamu wa mwili kabla ya safari ya kwanza ya chombo cha wanaanga kwenye Artemis II.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha