Jumba la Panda la Qatar lafunguliwa rasmi kwa umma

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 18, 2022
Jumba la Panda la Qatar  lafunguliwa rasmi kwa umma
Tarehe 17, Novemba, Panda “Si Hai”akiwa ndani ya Jumba la Panda katika Mji wa Doha, Qatar.(Mpiga picha:Pan Yulong/Xinhua)

Wakati siku ya kufunguliwa kwa Kombe la Dunia la Qatar la Mwaka 2022 ilipowadia, Panda “Jingjing” na “Si Hai” walionekana rasmi na umma huko Doha tarehe 17, Jumba la Panda katika bustani ya Al Khor huko Doha walioishi lilifunguliwa siku hiyo.

Kutokana na makubaliano kati ya China na Qatar, “Jingjing” na “Si Hai” wataishi nchini Qatar kwa miaka 15. “Jingjing” ni panda dume mwenye umri wa miaka minne, na "Sihai" ni panda jike mwenye umri wa miaka mitatu, wote walizaliwa katika Kituo cha Shenshuping cha Kituo cha Uhifadhi na Utafiti wa Panda cha Wolong cha China.Oktoba 19 mwaka huu, "Jingjing" na "Si Hai" walifika katika Doha kwa ndege maalum, na kupelekwa kwa gari maalum kwenye Jumba la Panda katika bustani ya Al Khor huko Doha. Baada ya hapo, panda hawa mbili waliwekwa karantini.

Balozi wa China nchini Qatar Zhou Jian alisema kuwa Qatar inatilia maanani sana ushirikiano kati ya China na Qatar katika utunzaji wa panda, Upande wa Qatar umejenga jumba kubwa la panda lenye mwanga mzuri, panda hawa wawili wamepata utunzaji mzuri baada ya kuishi huko.

Watu wa Qatar wameonesha shauku kubwa kwa ujio wa panda hawa. Siku ya kufunguliwa kwa jumba la panda, familia nyingi zilikuja kutembelea, wakati walipoondoka, watoto waliobeba wanasesere wa panda waliwaambia waandishi wa habari: "Asante China!"

Zhou Jian alisema kuwa ujio wa panda hawa wawili ni kabla ya kufunguliwa kwa Kombe la Dunia huko Qatar, siyo tu umebeba pongezi za Wachina kwa Kombe la Dunia huko Qatar, bali pia unaonesha uungaji mkono mkubwa wa serikali ya China kwa Qatar kuandaa Kombe la Dunia. Ninaamini kwamba mashabiki wanaokuja Qatar kutazama Kombe la Dunia, pia watakuja jumba hilo la panda kuwaangalia panda hao wanaopedeza."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha