Meli ya kale ya No.2 ya “Mlango wa Mto Changjiang” yaanza kuibuka kutoka kwenye maji

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 21, 2022
Meli ya kale ya No.2 ya “Mlango wa Mto Changjiang” yaanza kuibuka kutoka kwenye maji
Picha iliyopigwa tarehe 21, Novemba ikionesha meli ya kale “ikikumbatia ” meli ya uokoaji.

Kazi ya kuibua meli kamili ya kale ya No. 2 ya “Mlango wa Mto Changjiang”, ambayo ni meli kubwa zaidi ya ubao ya kale chini ya maji iliyogunduliwa katika utafiti wa mabaki ya kale ya China, imeanzishwa kwa mafanikio kwenye mlango wa Mto Changjiang tarehe 21. Kutokana na kuendelea kwa utaratibu kwa kazi hiyo, tarehe 21 asubuhi mapema, sehemu ya meli hiyo imeanza kuibuka kutoka kwenye uso wa maji ikionekana kwa watu. (Xinhua/Jin Liwang)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha