Ushirikiano kati ya China na Kituo cha Kimataifa cha Kuboresha Mahindi na Ngano wasaidia ongezeko la uzalishaji wa chakula

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2022
Ushirikiano kati ya China na Kituo cha Kimataifa cha Kuboresha Mahindi na Ngano wasaidia ongezeko la uzalishaji wa chakula
Picha hii iliyopigwa tarehe 7, Novemba ikionesha aina ya mbegu za mahindi kutoka Mexico kwenye makao makuu ya Kituo cha Kimataifa cha Kuboresha Mahindi na Ngano katika kitongoji cha Texcoco, Mexico.

Kituo cha Kimataifa cha Kuboresha Mahindi na Ngano kilianzishwa mwaka 1966, kikiwa ni kituo cha kimataifa cha utafiti na mafunzo kuhusu kilimo bila kutafuta faida. Hivi sasa karibu nusu ya mbegu za mahindi na ngano zilizopandwa katika nchi zinazoendelea duniani zinatolewa na kituo hicho.

Tangu China ilipoanzisha uhusiano wa wenzi wa utafiti na kituo hicho mwaka 1974, mashirika zaidi ya 20 za China yameshiriki kwenye mawasiliano ya mbegu nacho.

Kwa mujibu wa takwimu za kituo hicho, China imetoa aina za mbegu za ngano zaidi ya 1000 kwa bohari hilo la anuwai ya mazao ya kilimo. Tokea mwaka 2000, aina 13 mpya za mbegu za mahindi zilizooteshwa kwa ushirkiano wa China na kituo hicho zimepandwa katika nchi ya Nepal na nchi nyingine, zikisaidia ongezeko la uzalishaji wa chakula wa nchi hizo. (Picha zilipigwa na Zhu Yubo/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha