Saudi Arabia yaiduwaza Argentina kwenye mchezo wa Kundi C la Kombe la Dunia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 23, 2022
Saudi Arabia yaiduwaza Argentina kwenye mchezo wa Kundi C la Kombe la Dunia
Feras Albrikan (kati) wa Saudi Arabia akisalimiana na Lionel Messi (kulia) wa Argentina baada ya mechi ya Kundi C kati ya Argentina na Saudi Arabia kwenye Kombe la Dunia la FIFA Mwaka 2022 kwenye Uwanja wa Lusail mjini Lusail, Qatar, Novemba 22, 2022. (Xinhua/Li Ga)

LUSAIL - Saleh Alshehri na Salem Aldawsari wamefunga mabao ya kipindi cha pili wakati Saudi Arabia ilipoleta huzuni kubwa kwa kuifunga Argentina mabao 2-1 katika mechi yao ya Kundi C ya Kombe la Dunia la FIFA hapa Jumanne.

Lionel Messi aliifungia Argentina bao la kuongoza kwa kufunga penalti dakika ya 10 kabla ya Alshehri na Aldawsari kufunga mapema kipindi cha pili mbele ya mashabiki 88,000 kwenye uwanja wa Lusail, nchini Qatar.

Matokeo hayo yalihitimisha mfululizo wa kutofungwa kwa Argentina wa mechi 36 tangu michuano ya Copa America Mwaka 2019 nchini Brazil, ambapo walipoteza kwa waandaji wa michuano hiyo kwenye nusu fainali.

Ulikuwa ushindi wa kwanza kabisa wa Saudi Arabia dhidi ya timu hiyo ya Amerika Kusini na ushindi wao wa nne pekee katika mechi 17 za Kombe la Dunia kwa jumla.

Argentina, iliyofikiriwa na wengi kuwa moja ya timu zinazowania taji kabla ya michuano hiyo kuanza, sasa huenda ikahitaji kushinda mechi zao zote mbili za kundi zilizosalia dhidi ya Mexico na Poland ili kusonga mbele kwa raundi inayofuata.

Kila kitu kilionekana kuwa sawa kwa mabingwa hao mara mbili wa Kombe la Dunia wakati mwamuzi wa Slovenia Slavko Vincic alipotoa penalti katika dakika ya tisa baada ya Ali Albulayhi kumuangusha Leandro Paredes kwenye eneo la hatari.

Messi alimpeleka kipa Mohammed Alowais upande usiyo sahihi huku akiukwamisha mpira wavuni kwa utulivu.

Argentina ilifunga mabao matatu kwa kuotea katika kipindi cha kwanza - mara mbili kutoka kwa Martinez na moja kutoka kwa Messi - walipokuwa wakihangaika kutafuta njia ya kupita safu ya ulinzi ya Saudi Arabia.

Saudi Arabia hawakuwa na mkwaju hata mmoja katika dakika 45 za kwanza lakini hilo lilibadilika muda mfupi baadaye kwani vijana wa kocha Herve Renard waliibuka upya wakiwa na kikosi chenye nguvu zaidi.

Meneja wa Argentina Lionel Scaloni alijaribu kwa kubadilisha wachezaji mara tatu huku Enzo Fernandez, Julian Alvarez na Lisandro Martinez wakichukua nafasi za Paredes, Papu Gomez na Romero.

Mabadiliko yalionekana kuleta athari mara moja. Golikipa wa Saudi Arabia Alowais aliokoa mkwaju wa hali ya juu na kumnyima Martinez fursa ya kufunga kisha akazuia shuti la Angel Di Maria katika jaribio lake la pili.

Fowadi wa Manchester City, Alvarez alipata nafasi nyingine katika dakika ya 10 ya dakika za lala salama lakini mpira wake wa kichwa ukapanguliwa na Alowais.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha