Jumba la makumbusho ya sayansi lililojengwa na China lavutia mioyo ya Waethiopia wanaopenda sayansi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 24, 2022
Jumba la makumbusho ya sayansi lililojengwa na China lavutia mioyo ya Waethiopia wanaopenda sayansi
Picha hii iliyopigwa Tarehe 8 Novemba 2022 ikionyesha mwonekano wa ndani wa jumba jipya la makumbusho ya sayansi lililojengwa kwa msaada wa China na kuzinduliwa mjini Addis Ababa, Ethiopia. (Xinhua/Michael Tewelde)

ADDIS ABABA - Tewodros Eshetu alikuwa mmoja wa Waethiopia wa kwanza wapenda sayansi na teknolojia waliopanga foleni kwa saa nyingi kutazama jumba la makumbusho ya kisasa ya sayansi lililozinduliwa hivi majuzi.

"Katika nchi ambayo vifaa vinavyohusiana na sayansi na teknolojia ni kama havipo kabisa, haishangazi kuwa mmoja wa Waethiopia, haswa vijana, ambao walikuwa wakisubiri kwa hamu kwenye foleni kujionea makumbusho ya sayansi," Eshetu amesema, huku akisisitiza umuhimu mkubwa wa makumbusho hayo katika kukuza sayansi na teknolojia nchini Ethiopia.

Jumba hilo la makumbusho liliyosaidiwa na China lililopo Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, inasemekana kuwa jumba la makumbusho la kwanza kabisa barani Afrika linalohusu sayansi pekee.

Jumba hilo la makumbusho likiwa limejengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa hekta 6.78, lina majengo makuu mawili, lipo kwenye eneo la ardhi lenye ukubwa wa mita 15,000. Kituo hiki kina maonyesho kadhaa shirikishi ambayo yanaonyesha suluhisho katika huduma za afya, fedha, usalama wa mtandao, mifumo ya habari ya kijiografia (GIS), tasnia ya huduma, uchanganuzi wa data, utengenezaji na roboti, kati ya zingine.

Ethiopia, nchi ya pili barani Afrika kwa idadi kubwa ya watu ikiikaribia Nigeria, ilizindua jumba la makumbusho ya sayansi lenye umbo la kuba mwezi uliopita ili kutafakari mustakabali wa teknolojia katika mabadiliko ya kidijitali barani Afrika.

Katika wiki chache tu za kwanza tangu kifunguliwe, kituo hicho kimevutia mamia kwa maelfu ya Waethiopia, hasa vijana wanaoongezeka nchini humo.

Katika kipindi cha mwezi mmoja tangu kufunguliwa rasmi Tarehe 4 Oktoba, jumba la makumbusho ya sayansi la Ethiopia lilitembelewa na zaidi ya wapenda sayansi na teknolojia 700,000 kutoka Ethiopia na kwingineko, kwa mujibu wa takwimu kutoka Kituo cha Akili Bandia cha Ethiopia.

“Mimi nipo hapa kwa mara ya kwanza, nashangazwa sana na jengo hilo na hata dhana yake ya teknolojia na muunganisho wa kidijitali, hakika nashangaa sana,” amesema mmmoja wa watembeleaji wa makumbusho hiyo Manaye Ewnetu.

China yawezesha Ethiopia katika hitaji la Sayansi na Teknolojia

Akizungumza na Shirika la Habari la China, Xinhua hivi karibuni, Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Akili Bandia cha Ethiopia Worku Gachena amesema jumba hilo la makumbusho ya sayansi linaweza kuonekana kama dhihirisho la hivi punde la ushirikiano unaokua kati ya China na Ethiopia katika nyanja hiyo.

Mkurugenzi mkuu huyo amesema China haijaisaidia Ethiopia tu kupata jumba la makumbusho hiyo ya kisasa bali pia inawapa uwezo wataalam wa Ethiopia katika masuala ya akili bandia.

"Wachina wamekuwa wakiunga mkono sana teknolojia za akili bandia katika kujenga uwezo katika elimu na sekta nyingine," Gachena amesema.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha