Msaada waelekea eneo la Tetemeko la ardhi la Magharibi mwa Indonesia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2022
Msaada waelekea eneo la Tetemeko la ardhi la Magharibi mwa Indonesia
Tarehe 24, Novemba, 2022, mwanamke akiangalia waokozi wakitafuta mtoto wake kwenye magofu ya shule ya Kijiji cha Mangunkerta, Cianjur, Mkoa wa West Java wa Indonesia. (Xinhua/Veri Sanovri)

Ofisa mwandamizi Alhamisi alisema kuwa, chakula, dawa na vitu vingine vinavyohitajiwa na waathiriwa vimetengwa kwa eneo la tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 5.6 katika kipimo cha Richter kwenye Magharibi mwa Indonesia.

Mkuu wa Idara ya Taifa ya Usimamizi wa Maafa Suharyanto alisema, tetemeko kubwa la ardhi lililotokea kwenye Mkoa wa West Java limesababisha wakazi 62,545 kupoteza nyumba zao za kuishi kwenye eneo la Cianjur lililoathiriwa zaidi na tetemeko la ardhi. Kwa jumla vituo 14 vya uokoaji vimeanzishwa kwa hivi sasa.

Suharyanto alisema, vitendo vya kutafuta na kuokoa waathiriwa kwenye tetemeko la ardhi viliendelea Alhamisi, ambapo mtu mmoja aligunduliwa kufariki na idadi ya vifo imefikia 272, na wengine 39 bado hawajajulikana walipo.

“Mvua, njia nyembamba na sehemu zilizoko mbali kwenye eneo la tetemeko la ardhi vimezuia vitendo vya uokozi,” alisema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha