Richarlison aifungia Brazil mara mbili, huku penalti yenye utata ikimsaidia Ronaldo kuweka historia (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2022
Richarlison aifungia Brazil mara mbili, huku penalti yenye utata ikimsaidia Ronaldo kuweka historia
Alex Sandro (kati) wa Brazil akipiga mpira kwa kichwa kwenye mechi ya Kundi G kati ya Brazil na Serbia kwenye Kombe la Dunia la FIFA la 2022 kwenye Uwanja wa Lusail mjini Lusail, Qatar, Novemba 24, 2022. (Xinhua/Wang Lili)

DOHA - Mechi ya kwanza ya Brazili iliyokuwa ikingojewa kwa hamu katika Kombe la Dunia la 2022 ilimalizika Alhamisi kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Serbia huku Richarlison akifunga goli moja rahisi na goli lingine maridadi kumaliza upinzani mkali wa Serbia kwenye nusu ya pili.

Ingawa Brazil ilichezesha wachezaji watano washambuliaji na mabeki wa pembeni pia wakasonga mbele, kila walipoweza, timu hiyo inayopigiwa chapuo kuchukua taji mwaka huu haikuweza kupata njia kwenye ngome kali ya ulinzi ya Serbia hadi kulipokuwa na zaidi ya saa kuelekea mwisho wa mchezo.

Richarlison, ambaye bado hajafunga bao kwenye Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu akiwa na Tottenham Hotspurs, alifunga goli la kwanza baada ya kipa wa Serbia, Vanja Milinkovic-Savic kupangua kombora kutoka kwa Vinicius Jr.

Bao lake la pili lilikuwa kazi ya sanaa alipokuwa akidhibiti, kupinda na kupiga shuti kwa mtindo wa sarakasi kuuweka mpira nje ya uwezo wa kipa Milinkovic-Savic.

Katika mechi nyingine, Breel Embolo wa Switzerland alifunga dhidi ya nchi aliyozaliwa wakati Switzerland ikiendeleza rekodi yake ya ajabu katika mechi ya ufunguzi wa kampeni za Kombe la Dunia kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Cameroon.

Switzerland haijawahi kupoteza mechi yao ya ufunguzi katika hatua ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia tangu Mwaka 1966.

Korea Kusini na Uruguay zilifungua dimba lao la Kundi H kwa sare ya nne ya 0-0 kwenye michuano hiyo, lakini hiyo haimaanishi kuwa ulikuwa mchezo mwepesi kwani pande zote zilikuwa na nafasi ya kutwaa pointi zote tatu.

Mchezo wa pili wa Kundi H uliingia utata dakika ya 63 baada ya Cristiano Ronaldo kupata na kufunga penalti yenye utata na kuifanya timu yake ya Ureno kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Ghana. Goli hilo la Ronaldo limemfanya aweke rekodi ya kufunga katika michuano mitano mfululizo ya Kombe la Dunia.

Andre Ayew aliisawazishia Ghana kwa shuti kali, lakini mabao ya haraka-haraka kutoka kwa Joao Felix na Rafael Leao yalifanya matokeo kuwa 3-1 dakika ya 80 kabla ya Osman Bukari kufanya matokeo kuwa 3-2 dakika ya 89 na Inaki Williams kukaribia kusawazisha dakika ya mwisho ya mchezo.

Michuano hiyo inaendelea leo Ijumaa kwa michezo ya raundi ya pili, ambapo katika Kundi A wenyeji Qatar watavaana na wawakilishi wa Afrika, Senegal huku Netherlands ikichuana na Ecuador. Pia kutakuwa na michezo ya Kundi B ambapo Wales itacheza na Iran, huku Marekani na Uingereza zikifunga michezo ya siku.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha