Maonyesho ya Mashujaa wa Terracotta yaangazia uhusiano wa kitamaduni kati ya China na Japan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 25, 2022
Maonyesho ya Mashujaa wa Terracotta yaangazia uhusiano wa kitamaduni kati ya China na Japan
Mtembeleaji akitazama maonyesho kwenye ziara ya waandishi wa habari katika maonyesho ya "Mashujaa wa Terracotta na China ya Kale: Urithi kutoka kwa Enzi ya Qin na Han" kwenye Jumba la Makumbusho ya Kifalme la Ueno huko Tokyo, Japani, Novemba 21, 2022. Katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Japan, maonyesho hayo yamefunguliwa hivi karibuni kwenye Jumba la Makumbusho ya Kifalme la Ueno mjini Tokyo, hatua ya mwisho ya maonyesho yake ya takriban mwaka mzima ya kusafiri nchini Japan. (Xinhua/Yang Guang)

TOKYO - Katika kuadhimisha miaka 50 tangu kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Japan, maonyesho ya "Mashujaa wa Terracotta na China ya Kale: Urithi kutoka kwa Enzi ya Qin na Han" yamefunguliwa hivi karibuni kwenye Jumba la Makumbusho ya Kifalme la Ueno mjini Tokyo, hatua ya mwisho ya maonyesho yake ya takriban mwaka mzima ya kusafiri nchini Japan.

"Nadhani Mashujaa wa Terracotta wanapaswa pia kuitwa mabalozi, kwa sababu wao, kama panda, wanaweza kuwafanya watu kuhisi haiba ya China popote wanapoenda," mwanahistoria wa Japan na profesa wa heshima wa Chuo Kikuu cha Gakushuin Kazuyuki Tsuruma amesema.

Mwaka 1974, baada ya sanamu za jeshi la Terracotta kugunduliwa, zilisababisha hisia duniani kote. Mwaka 1976, maonyesho ya kwanza ya nje ya China ya Mashujaa wa Terracotta yalifanyika Japani.

Tang Qishan, msimamizi wa maonyesho ya sasa na mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Utamaduni la Japan na China, amesema, "Wakati huo, watu wapatao milioni 1.5 walipanga foleni kutembelea Jumba la Makumbusho ya Taifa la Tokyo. Umaarufu haukuwa mdogo kuliko ule wa panda kuja Japan."

Tang anasema anatumai kuwa watu wa Japan wanaweza kujifunza kuhusu utamaduni wa ajabu wa enzi za Qin na Han za China kupitia maonyesho hayo, na pia kudurusu historia ya mabadilishano ya kitamaduni ya China na Japan Mwaka 1976.

Maonyesho ya awali huko Kyoto, Shizuoka na Nagoya yamekuwa na mafanikio makubwa ambapo tayari kuna watembeleaji 240,000, Tang amesema na kuongeza kuwa "Kinachotufurahisha zaidi ni kwamba kuna vijana wengi kati ya watazamaji. Tumeridhika sana na shauku iliyoonyeshwa na vijana wa Japani kwa utamaduni wa China wa Qin."

Yakiwa na jumla ya seti 121 za mabaki ya kitamaduni kutoka taasisi na makumbusho ya kitamaduni katika mikoa ya Shaanxi na Hunan nchini China, maonyesho hayo makubwa yamegawanywa katika sehemu tatu za "Qin katika mkesha wa kuungana tena, kuzaliwa kwa enzi iliyoungana, na mafanikio ya Enzi ya Han."

Sanamu za mashujaa na farasi, vitu vya kale vya mawe, bidhaa za shaba na vionyeshwa vingine kwenye maonyesho vinaanzia kutoka kwa Enzi ya Zhou Magharibi hadi Enzi ya Han ya Mashariki. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha