Njia ya kwanza ya safari za ndege za mizigo yafunguliwa katika uwanja wa ndege wa kwanza maalumu kwa mizigo wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2022
Njia ya kwanza ya safari za ndege za mizigo yafunguliwa katika uwanja wa ndege wa kwanza maalumu kwa mizigo wa China
Picha hii iliyopigwa Novemba 27, 2022 ikionyesha ndege ya kubeba mizigo pekee kutoka Shenzhen ikipakuliwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Huahu huko Ezhou, Mkoa wa Hubei katikati mwa China. Uwanja wa ndege wa kwanza wa mizigo wa China katika Mji wa Ezhou, Mkoa wa Hubei nchini China, Jumapili umezindua njia yake ya kwanza ya ndege za mizigo pekee, inayounganisha Ezhou na Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China. Uwanja wa ndege wa Ezhou Huahu pia ni wa kwanza kwa ndege za mizigo barani Asia na wa nne wa aina yake duniani. Tangu uwanja huo wa ndege uanze kutumika Julai 17 mwaka huu, umefungua njia nyingi za ndege za abiria zinazounganisha Ezhou na miji mingine ikiwa ni pamoja na Beijing, Shanghai, na Xiamen. Mamlaka za uwanja huo zimesema, uwanja huo pia utafungua njia ya anga ya ndege za mizigo pekee inayounganisha Ezhou na Shanghai hivi karibuni. (Xinhua/Wu Zhizun)

WUHAN - Uwanja wa ndege wa kwanza kwa ndege za mizigo wa China katika Mji wa Ezhou, Mkoa wa Hubei nchini China, Jumapili umezindua njia yake ya kwanza ya ndege za mizigo pekee, inayounganisha Ezhou na Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China.

Uwanja wa ndege wa Ezhou Huahu pia ni wa kwanza kwa ndege za mizigo barani Asia na wa nne wa aina hiyo duniani.

Tangu uwanja huo wa ndege uanze kutumika Julai 17 mwaka huu, umefungua njia nyingi za ndege za abiria zinazounganisha Ezhou na miji mingine ikiwa ni pamoja na Beijing, Shanghai, na Xiamen.

Kwa mujibu wa uwanja wa ndege huo, njia ya anga ya ndege za mizigo pekee inaendeshwa na ndege ya mizigo ya Boeing 737, inayobeba vifurushi. Njia hiyo ya anga inajumuisha maeneo kama vile Wuhan, Ezhou, Huangshi, na Huanggang katika Mkoa wa Hubei.

Mamlaka za uwanja zimesema, uwanja huo pia utafungua njia ya anga ya ndege za mizigo pekee inayounganisha Ezhou na Shanghai hivi karibuni.

Uwezo wa shehena ya kila mwaka ya mizigo na vifurushi katika uwanja huo wa ndege unatarajiwa kufikia tani milioni 3.3 ifikapo Mwaka 2030, na kiwango cha abiria cha kila mwaka kufikia milioni 1.5. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha