Visima vinavyotumia nishati ya jua vinavyofadhiliwa na China vyasaidia kukabiliana na msongo wa maji katika ardhi kame nchini Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 28, 2022
Visima vinavyotumia nishati ya jua vinavyofadhiliwa na China vyasaidia kukabiliana na msongo wa maji katika ardhi kame nchini Kenya
Watu wakichota maji kwenye kisima cha maji kinachotumia nishati ya jua katika Kaunti ya Machakos, Kenya, Novemba 23, 2022. (Picha na Naftali Mwaura/Xinhua)

NAIROBI - Uso wa Winifred Nzioka unaonekana kung'aa wakati mkulima mmoja alipopelekea madumu kadhaa ya maji kwenye boma lake alasiri tulivu ili kukata kiu ya ng'ombe wenye kudhoofu.

Mama huyo makamo mwenye watoto watano amejenga nyumba ya kudumu katikati ya mashamba yaliyochomwa na jua katikati mwa Kaunti ya Machakos, Kusini mwa Kenya, ambayo iko katika hali ya ukame wa muda mrefu.

Umbali wa mita chache kutoka kwa boma la Nzioka ni shule ya umma ambapo kisima cha maji kinachotumia nishati ya jua kinachofadhiliwa na mjasiriamali wa China kinatoa ahueni kwa msongo wa maji uliokuwa ukiwatesa wakaazi wa uwanda kame ulio karibu na Kaunti ya Machakos.

Mkulima huyo mdogo ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua wakati wa mahojiano ya hivi majuzi kwamba shida za maji sasa ziko nyuma yake kwani anaweza kuteka “bidhaa hiyo” kutoka kwa kisima kinachotumia nishati ya jua kwa malipo kidogo.

“Nimenufaika sana na kisima cha maji ambacho napata maji kwa ajili ya ng’ombe wangu na matumizi ya nyumbani, tuna furaha kwa sababu maji safi ya kunywa sasa yapo mlangoni kwetu,” anasema Nzioka.

Kikiwa kilikamilika kujengwa Mwezi Mei mwaka huu, kisima hicho kinachotumia nishati ya jua katika Shule ya Msingi ya Kwakatheke, iliyo karibu na nyumba ya Nzioka, ni wazo la Li Xia, afisa mkuu mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Kampuni ya Nishati ya Jua ya Shenzhen.

Kupitia ushirikiano na vikundi vya nchini Kenya visivyotafuta faida, Li ametumia suluhu za nishati ya jua kukabiliana na msongo wa maji huko Machakos na maeneo kame ya Kenya yanayokabiliwa na ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Li, ambaye amewasili siku chache tu kutoka Misri ambako alihudhuria mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa, anasema kutumia nishati ya jua kusukuma maji kutoka kwenye visima vya kuchimba kunasaidia kukabiliana na hali inayozidi ya uhaba wa rasilimali hiyo katika maeneo ya Afrika yenye matatizo makubwa yanayotokana mabadiliko ya tabianchi.

Fabian Daniel, ambaye ni mkulima mwenye umri wa miaka 18, anaonekana katika eneo lake akiongoza ng'ombe wawili ambao wamebeba madumu ya lita 20 yaliyojaa maji yaliyochotwa kutoka kwenye kisima kinachohudumiwa maji yake na kisima kinachotumia nishati ya jua.

"Tulikuwa tukitembea takribani kilomita tano na kutumia zaidi ya saa mbili kufika kwenye chanzo cha maji, lakini siyo hivyo, sasa tunapata bidhaa kwenye kibanda hiki kilicho mlangoni kwetu," anasema Daniel.

Hadi kufikia Mwezi Mei mwaka huu zaidi ya lita milioni tano za maji safi ya kunywa zimefikishwa kwa kaya tangu kukamilika kwa mradi huo wa kisima kinachotumia nishati ya jua na kioski, anasema Tajinder Singh, mkurugenzi mkuu wa Project Maji, shirika lisilo la faida la kijamii ambalo limeshirikiana na Li kukabiliana na matatizo ya maji nchini Kenya.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha