Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Jua wa China wafanya Kombe la Dunia bila kuleta uchafuzi zaidi kwa Mazingira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2022
Mradi wa Kuzalisha Umeme kwa nishati ya Jua wa China wafanya Kombe la Dunia bila kuleta uchafuzi zaidi kwa Mazingira
Pichi ikionesha kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua Al Kharsaaha. (Picha/China Daily)

Tangu Kombe la Dunia 2022 lilipofunguliwa kwenye Uwanja wa Michezo wa Al Bayt huko Doha, Qatar Tarehe 20, Novemba, nishati safi ya umeme iliyozalishwa kwenye kituo cha umeme wa nishati ya jua kilichojengwa na kampuni ya China imekuwa ikichangia kithabiti michezo ya dunia.

Mradi wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua Al Kharsaaha wenye uwezo wa Megawati 800 ni kituo cha kwanza cha umeme kisichotumia nishati ya visukuku nchini Qatar, na kilijengwa na Kampuni ya PowerChina Guizhou yenyewe.

“Utoaji wa kaboni unaopungua wa mradi huo utakuwa sawa na nusu ya ule wa wakati wa Kombe la Dunia,” alisema meneja wa mradi huo Wei Yujin. “Inakadiriwa mradi huo utatoa nishati safi ya umeme ya bilioni 1.8 khw hivi kwa Qatar kila mwaka, ambayo itakidhi mahitaji ya familia 300,000 nchini humo.”

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha