Mwanabiolojia wa New Zealand aelezea safari ya kwenda eneo lenye kina kirefu la bahari kama "ajabu"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 29, 2022
Mwanabiolojia wa New Zealand aelezea safari ya kwenda eneo lenye kina kirefu la bahari kama
Marubani wanaoweza kuzama chini ya maji Deng Yuqing (kati) na Yuan Xin (kushoto) kutoka Taasisi ya sayansi na uhandisi ya Bahari ya Kina Kirefu (IDSSE) katika Akademia ya Sayansi na Uhandisi ya China, na Mwanabiolojia wa Bahari wa New Zealand Dk. Kareen Schnabel kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Maji na Mazingira ya New Zealand wakijitayarisha kwa safari yao ya kuelekea Kermadec Trench kwenye meli ya utafiti ya China Tansuoyihao, Novemba 4, 2022. (Chen Kunxin/IDSSE/Handout kupitia Xinhua)

AUCKLAND, New Zealand - Mwanabiolojia wa baharini wa New Zealand Dk. Kareen Schnabel kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Maji na Mazingira (NIWA) Jumapili alitumia neno "ajabu" mara nyingi kuelezea uzoefu wake wa kipekee na wenzake wa China kwa kutumia chombo cha kubeba binadamu kwenye kina kirefu cha maji (HOV) Fendouzhe baada ya safari yao katika mojawapo ya maeneo yenye kina kirefu zaidi baharini siku ya Jumapili.

Upigaji mbizi huo wenye mafanikio ulifanywa pamoja na Schnabel na marubani wa chini ya maji Deng Yuqing na Yuan Xin kutoka Taasisi ya Sayansi na Uhandisi wa Bahari ya Kina (IDSSE) ya Akadamia ya Sayansi ya China.

Katika safari hiyo, Schnabel na Deng wamekuwa wanawake wa kwanza kushuka chini kwenye Scholl Deep kwenye Mkondo wa Kermadec.

Ilikuwa ni ziara ya pili pekee ya wafanyakazi kuchunguza Scholl Deep ya Mkondo wa Kermadec na ilifanywa kama sehemu ya safari ya kisayansi ya miezi miwili kwenye meli ya utafiti ya IDSSE Tansuoyihao.

Scholl Deep ndiyo sehemu ya kina kabisa inayojulikana ya Mkondo wa Kermadec, umbali wa zaidi ya kilomita 1,000 Kaskazini Mashariki mwa New Zealand. Mkondo huo una urefu wa zaidi ya kilomita 1,000 na sehemu yake ya kina kirefu zaidi ina urefu zaidi ya Mlima Qomolangma.

Kwa kutumia chombo cha Fendouzhe, wanasayansi hao walikusanya sampuli za maji, mchanga, mawe, sampuli za kibayolojia na data za mazingira ya bahari yenye kina kirefu.

Dk. Schnabel na marubani wa chini ya maji walitumia saa sita chini ya bahari kuchunguza Scholl Deep na pande za mwinuko za mfereji.

"Inafurahisha sana kwa wanasayansi wa China na New Zealand kupata fursa ya kufahamu kwa kina utata na utofauti wa jiografia na mfumo wa ikolojia wa Mkondo wa Kermadec," Dk. Peng Xiaotong, kiongozi wa safari hii kutoka IDSSE amesema.

Balozi wa China nchini New Zealand, Wang Xiaolong ameielezea safari hiyo kuwa safari ya uchunguzi, urafiki na pia kutafuta ushirikiano, ambayo inatoa jukwaa muhimu la ushirikiano wa baharini kati ya China na New Zealand.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha