China yarusha kwenye anga ya juu Chombo cha Shenzhou-15, ikilenga kupokezana majukumu kwa wanaanga kwenye anga ya juu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Novemba 30, 2022
China yarusha kwenye anga ya juu Chombo cha Shenzhou-15, ikilenga kupokezana majukumu kwa wanaanga kwenye anga ya juu
Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15, kilicho juu ya roketi ya Long March-2F Y15, kikiruka kutoka kwenye Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Novemba 29, 2022. (Xinhua/Li Gang)

JIUQUAN - China imerusha chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-15 Jumanne usiku, kikiwa na wanaanga watatu ndani yake ambao watakutana na wenzao kwenye kituo cha anga ya juu cha nchi hiyo na kufanya makabidhiano ya kazi.

Chombo hicho, kilicho juu ya roketi ya Long March-2F Y15, kilirushwa kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China saa 11:08 jioni kwa Saa za Beijing, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA).

Takriban dakika 10 baada ya kurushwa, chombo cha Shenzhou-15 kilijitenga na roketi na kuingia kwenye njia yake iliyopangwa. Wananaanga katika chombo hicho wako katika hali nzuri na urushaji umekuwa wenye mafanikio kamili, CMSA imetangaza.

Baada ya kuingia kwenye obiti, chombo hicho cha anga ya juu cha Shenzhou-15 kitafanya minyumbuliko ya haraka na ya kiotomatiki pamoja na kuungana pamoja na kituo cha angani.

Wanaanga hao wa Shenzhou-15, kwa mara ya kwanza katika historia ya anga ya juu ya China, watapokezana majukumu na wanaanga wengine walioko kwenye chombo cha Shenzhou-14, ambao walitumwa kwenye kituo cha anga ya juu mwezi Juni, imesema CMSA.

Wakati wa misheni yao, wanaanga wa Shenzhou-15 watafanya majaribio yanayohusiana na makazi ya muda mrefu katika kituo cha anga ya juu cha China katika usanidi wake wa moduli tatu, Ji Qiming, msaidizi wa mkurugenzi wa CMSA, alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumatatu.

Wanaanga hao pia watafungua, kufunga na kupima kabini 15 za majaribio ya kisayansi, na kufanya majaribio ya kisayansi zaidi ya 40 katika nyanja za utafiti na matumizi ya sayansi ya anga, dawa za anga na teknolojia ya anga, Ji amesema.

Hii ni safari ya 27 ya vyombo vya anga ya juu tangu mpango wa anga ya juu wa China kuidhinishwa na kuanzishwa, na ni ujumbe wa nne wa wanaanga wa mradi wa kituo cha anga ya juu cha China.

Mafanikio ya urushaji huu yanaashiria kukamilika kwa misheni zote 12 za urushaji zilizopangwa katika hatua muhimu za uthibitishaji wa teknolojia na ujenzi wa kituo cha anga ya juu cha China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha