Magari yanayotumia nishati ya umeme (EV) yanayoundwa China yang'aa kwenye maonyesho ya magari ya Thailand

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 02, 2022
Magari yanayotumia nishati ya umeme (EV) yanayoundwa China yang'aa kwenye maonyesho ya magari ya Thailand
Watembeleaji wa maonyesho wakitazama gari linalotumia nishati ya umeme linaloonyeshwa kwenye Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Thailand 2022 huko Bangkok, Thailand, Desemba 1, 2022. Maonyesho hayo ya Magari yameanza Alhamisi na yataendelea hadi Desemba 12. (Xinhua/Wang Teng)

BANGKOK - Maonyesho ya Kimataifa ya Magari ya Thailand, yaliyoanza Alhamisi, yamevutia idadi kubwa ya waundaji magari wa China wakionyesha modeli zao za hivi punde za magari yanayotumia nishati ya umeme (EV).

Huku motisha mpya za EV zikifanya kazi kwa zaidi ya miezi sita, soko la EV nchini China limeshuhudia mzunguko wa maendeleo ya haraka kutokana na punguzo kubwa la kodi na ruzuku.

Katika maonyesho ya mwaka huu, chapa kuu za kimataifa zimechukua EV kama vivutio vyao vya maonyesho, na karibu nusu ya modeli za EV pekee zikiwa ni chapa za China.

Yakionyeshwa kwa mara ya kwanza katika soko la Thailand, magari ya Ora Grand Cat yanayoundwa na Kampuni ya Great Wall Motor (GWM) yamevutia umati wa watembeleaji wa maonyesho kwa muundo na mwonekano wa mtindo.

GWM imeleta jumla ya modeli saba za magari kwenye maonyesho hayo, zikiwemo modeli tatu za EV pekee, pamoja na magari yanayouzwa vizuri kama vile Haval H6 Hybrid, ambayo ilitumika kama moja ya magari rasmi ya usafiri kwa ajili ya Mkutano wa Viongozi wa Nchi za Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki (APEC) mwezi Novemba. .

Tangu kuanzishwa kwa kiwanda nchini Thailand mwishoni mwa Mwaka 2020, GWM imezindua modeli tano za magari ya nishati mchanganyiko na EV pekee, zinazokidhi mahitaji mbalimbali ya ndani kama vile masafa tofauti ya bei, Mkuu wa GWM katika eneo la ASEAN na Thailand Elliot Zhang ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Kampuni ya SAIC Tawi la Thailand nayo imeleta modeli tisa kwenye maonyesho, hayo ikiwa ni pamoja na modeli tatu halisi za EV , kati ya hizo MG4 ni gari la kwanza linalotumia nishati ya umeme nyuma-gurudumu lililozinduliwa katika soko la Kusini-Mashariki mwa Asia.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo ya kuunda magari ya China, modeli hiyo mpya inaweza kutoa uzoefu bora wa kuendesha gari ikilinganishwa na modeli kama hizo katika suala la udhibiti na uthabiti, na imepata maoni mazuri kutoka kwa watumiaji wengi wa majaribio wa nchini Thailand.

Maonyesho hayo ya magari ya kila mwaka, ambayo yataendelea hadi Desemba 12, yamevutia waundaji magari 35 na chapa 17 za pikipiki kutoka zaidi ya nchi na maeneo 10.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha