Duka la kwanza la vitabu kwa Walemavu lafunguliwa Shanghai

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2022
Duka la kwanza la vitabu kwa Walemavu lafunguliwa Shanghai
Mkazi akijifunza lugha ya ishara ya mikono kwenye duka la vitabu kwa walemavu tarehe 4, Desemba. (Picha/Chinanews)

Tarehe 3, Desemba, duka la kwanza la vitabu la Shanghai kwa walemvu lilifunguliwa kwenye Nyumba No.226 ya Mtaa wa Nanchang mjini Shanghai. Duka hilo liliendeshwa na Kampuni ya Xinhua ya Shanghai, Shirikisho la Walemavu la Shanghai pamoja na Ofisi ya usimamizi ya Mtaa wa Pili wa Ruijin kwenye eneo la Huangpu la Shanghai. Duka hilo likiwa na eneo la mita za mraba 37 tu, linaonyesha ipasavyo utoaji wa huduma kwa walemavu wa macho katika kila sehemu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha