Wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-14 cha China warudi salama duniani, na kutimiza shughuli nyingi za "kwanza"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 05, 2022
Wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-14 cha China warudi salama duniani, na kutimiza shughuli nyingi za
Chombo cha kurejea duniani cha Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 kikitua ardhini kwa usalama kwenye eneo la kutua la Dongfeng, katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazni mwa China, Desemba 4, 2022. (Xinhua/Li Gang)

BEIJING - Wanaanga watatu wa China waliokuwa kwenye chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14 wamerejea Duniani salama siku ya Jumapili, baada ya kutimiza majukumu mengi "ya kwanza" wakati wa misheni yao ya miezi sita kwenye kituo cha anga ya juu.

Chombo cha kurejea duniani cha Chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-14, kilichokuwa kimewabeba wanaanga Chen Dong, Liu Yang na Cai Xuzhe, kilitua kwenye eneo la kutua la Dongfeng, katika Mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China saa 2:09 usiku saa za Beijing, kwa mujibu wa Shirika la Anga ya Juu la China.

Wanaanga wote wako katika hali nzuri ya kimwili, na misheni ya Chombo cha Shenzhou-14 iliyosimamiwa na watu ilikuwa na mafanikio kamili, shirika hilo limetangaza.

Wanaanga hao mara baada ya kutua walibebwa na wafanyakazi wa ardhini na kuwekwa kwenye viti. Walionekana wakiwa watulivu na kuwapungia mkono wafanyakazi wa ardhini.

"Karibu tena nyumbani," watu waliwashangilia wananga hao watatu, huku wengi wakiinua kamera zao ili kunasa tukio hilo la kihistoria.

"Nimefurahi kushuhudia uundaji wa usanidi wa msingi wa kituo chetu cha anga ya juu," amesema Chen, kamanda wa misheni, pia mwanaanga wa kwanza wa China kukaa kwenye obiti kwa zaidi ya siku 200. "Ninajivunia nchi yangu."

Liu, mwanaanga wa kwanza wa kike wa China, amesema amepata kumbukumbu isiyoweza kusahaulika katika kituo cha anga ya juu na anafurahi kurudi katika nchi mama.

Chombo cha kurejea cha Shenzhou-14 kilichobeba wanaanga hao kilitenganishwa na Chombo cha Shenzhou-14 saa 1:20 jioni, Jumapili chini ya komandi ya Kituo cha Udhibiti wa Anga ya juu cha Beijing.

Mara tu baada ya chombo cha kuwarudisha kutua, timu ya kutafuta ardhini ilifika kwenye eneo la kutua. Wahudumu wa afya wamethibitisha kuwa wanaanga hao wako kwenye afya njema.

Ni mara ya kwanza kwa chombo cha anga za juu cha China kurudi kwenye eneo la kutua la Dongfeng usiku wa majira ya baridi. Kwa mujibu wa shirika hilo, "hali ya kurudi haraka" ambayo Shenzhou-14 ilitumia ilisababisha raundi chache kuzunguka obiti na kufupisha muda wa kurudi kwa chombo.

Timu ya watafiti ya China pia imeunda teknolojia nyingi za kibunifu ili kuwasaidia wanaanga wa Chombo cha Shenzhou-14 kuondokana na changamoto za joto la chini na usiku wa giza.

Wanaanga hao watatu walienda kwenye kituo cha anga ya juu Juni 5 mwaka huu. Wamekamilisha kazi nyingi wakati wa misheni yao, ikiwa ni pamoja na kusimamia minyumbuliko mitano, kufanya shughuli tatu za ziada, kutoa mihadhara ya sayansi ya moja kwa moja duniani kutokea anga ya juu, na kufanya majaribio kadhaa ya kiteknolojia.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha