Maonyesho ya Sanaa za Panda yafanyika ili kutoa wito wa kulinda anuwai ya viumbe

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 07, 2022
Maonyesho ya Sanaa za Panda yafanyika ili kutoa wito wa kulinda anuwai ya viumbe
(Picha inatoka vip.people.com.cn)

Hivi karibuni, “Maonyesho ya Panda 1864” yalifanyika kwenye Uwanja wa Zhengda wa Shanghai, China, ambapo sanaa za panda zilizotengenezwa kwa karatasi zaidi ya 500 zinaonekana kwenye uwanja huo, zikivutia macho ya watu.

Habari zilisema kuwa, maana ya “1864” ni idadi ya panda pori kutokana na uchunguzi wa nne wa panda. Maonyesho hayo pia yanaonesha hali halisi ya maisha ya panda pori na “wenzao”, kufahamisha ujuzi kuhusu kulinda anuwai ya viumbe, na maonesho hayo yamevutia watu wengi kusimama na kuangalia. Habari zinasema, maonyesho hayo yataendelea hadi tarehe 14, Desemba.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha