Kampuni ya China yazawadia Shule ya Zimbabwe majengo ya Masomo (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2022
Kampuni ya China yazawadia Shule ya Zimbabwe majengo ya Masomo
Mwanafunzi akiandika darasani kwenye shule ya msingi ya Vhuta katika eneo la Goromonzi, Zimbabwe. (Picha/Xinhua)

Kampuni moja ya China imeikabidhi shule moja ya Zimbabwe majengo mawili ya masomo pamoja na samani zao, zikiwa ni sehemu ya hatua za kampuni hiyo za kubeba wajibu wake wa kijamii katika kuboresha hali ya elimu ya sehemu hiyo nchini humo.

Majengo hayo mawili yalitolewa na Prospect Lithium Zimbabwe, tawi la Kampuni ya Cobalt ya Zhejiang Huayou nchini Zimbabawe, na yalizawadia Shule ya msingi ya Vhuta kwenye eneo la Goromonzi lililopo karibu na Harare, mji mkuu wa Zimbabwe. Kampuni hiyo pia imezizawadia shule nyingine zilizoko karibu nayo jengo la masomo lililokarabatiwa upya, mabweni ya walimu, samani za shule na vitabu vya masomo.

Kabla ya kujenga upya na kukarabati majengo yake, shule ya msingi ya Vhuta ilikabiliwa na matatizo ya upungufu wa madarasa ya masomo , hivyo elimu ya watoto imeathiriwa.

Mwalimu wa shule ya Vhuta Hilary Manyanga alisema, zawadi hiyo itasaidia kuboresha sifa ya elimu ya shule hiyo.

“Tunashukuru sana zawadi tuliyopata. Hapo kabla tulitoa mafunzo kwa njia ya kuchanganya wanafunzi wa mwaka tofauti, ambapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza, wa pili na wa tatu wanasoma katika darasa moja, lakini hivi sasa wanafunzi wa kila mwaka wana darasa lao wenyewe,” Manyanga aliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha